Zinazobamba

MAGUFULI ATUMBUA JIBU HILI LEO,SOMA HAPO KUJUA



Prof. William Lyakurwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Benki ya Maendeleo ya TIB
FALSAFA ya Rais John Magufuli ‘tumbua jipu’ inaendelea ambapo leo, amemtubua Prof. William Lyakurwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Benki ya Maendeleo ya TIB, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa, Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuchukua nafasi hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba Prof. Lyakurwa aliyekuwa mwenyekiti katika bodi hiyo kwa miaka mitatu.

“… ametenguliwa kutokana na mamlaka aliyonayo rais chini ya kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act),” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na mabadiliko hayo Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango  ametengua uteuzi wa wajumbe wa benki hiyo.

“Dk. Mpango, kutokana na mamlaka aliyonayo kupitia kifungu cha 9 (1) cha sheria ya mashirika ya Umma amewateua Brigedia 
Generali Mabula Mashauri, Dk. Razack B. Lokina, Bi. Rose Aiko, Prof. Joseph Bwechweshaija, Said Seif Mzee, Dk. Arnold Kihaule, Maduka Paul Kessy, Charles Singili kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo kuanzia leo,” imeeleza taarifa hiyo.

Hakuna maoni