Zinazobamba

WANAFUNZI WALIOFUKUZWA UDOM WAMJIBU RAIS MAGUFULI,WAIBUKA NA KUJIBU HOJA YA "VILAZA"SOMA HAPO KUJUA





NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kutangaza kuwa wanafunzi 7802 waliofukuzwa kwenye chuo kikuu cha Dodoma kuwa ni “vilaza” na hawana sifa za kuwepo chuoni hapo huku  akitakiwa kujiunga kwenye vyuo vyenye hadhi yao.

Hatimaye nao wanafunzi hao wameibuka na kusema wanasifa stahiki za kuwepo chuoni hapo,kutokana na kukidhi sifa ziliotangazwa na serikali kwa wanafunzi ambao wanatakiwa kusoma chuo hicho.

Akizungumza  na Waaandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wanafunzi hao,Ibrahim Abdallah amesema wao wanasikitishwa na kauli ya Rais Magufuli kwa kusema Rais atakuwa anapotoshwa juu ya suala hilo kutokana na wanafunzi wote waliopo hapo wanasifa ambazo zilitangwana Serikali.

Amesema sifa za udahili kwa wahitumu wa kidato cha nne tu ambao wametapa daraja la 1,2 na 3 huku akitakiwa amefahulu kwa alama A au B kwenye kwa masomo ya Sayansi.

Amesema licha ya serikali kutoa sifa hizo pia bado walitoa nafasi kwa hata wanafunzi wa kidato cha nne ambao walipata darala la nne ambao wao walitakiwa kusoma kozi maalum ya Cheti kabla ya kujiunga na ngazi Stashahada katika chuo hicho.

Hata hivyo,Mwanafunzi huyo aliendelea kueleza kwa uchungu amesema wanasikitishwa na hatua ya kukatishwa masomo yao huku bado wanafunzi wengine ambao walikuwa wanatakiwa kumaliza masomo yao ndani ya  mwezi huu sita jambo  analodai hawana pakwenda kutokana na ndoto yao yote ikiwa imepotea.
Hatahivyo,amesema hata kama Rais Magufuli ameona mfumo huo wa kuwasomesha wanafunzi wa masomo ya Sayansi ulikuwa hauna tija,angetakiwa kuuangalia jisni gani ya kuweza kuwasaidia wanafunzi kuriko hatua iliyochukuliwa na kuwafukuza wote wanafunzi hao.,
Ameleeleza kuwa hata hoja ya Rais anayodai kuwa kuna watoto wa Vigogo waliofeli ambao wamepenyezwa katika chuo hapo,wamesema anatakiwa kuwashughulikia watendaji waliohusika kuwapitisha wanafunzi hao kuriko kuishia kuwahusishwa wanafunzi wote huku akidai wengi wa wanafunzi hao ni masikini.
Katika Hatua nyingine wanafunzi hao wamemuomba Rais Magufuli kuangalia kwani wengi wao wanatoka kwenye Familia masikini.

1 comment

A.KSh said...

Vilaza ni vilaza tu, kutoka familia masikini hakumfanyi mwanafunzi kilaza akawa bora darasani, tunamuunga mkono mh.Rais wanafunzi wa aina hii wote OUT