CHADEMA KUITEKA NCHI,SOMA HAPO KUJUA
![]() | |
| Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila |
MKAKATI wa
kuteka nchi unapangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),anaandika Happiness Lidwino.
Ni kwa kufanya ziara nchi nzima
kwa lengo la kukukumbusha wananchi kwamba, nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu
wa Katiba ya Jamhuri.
Kumekuwepo
na malalamiko kwamba, Rais John Magufuli anaendesha nchi kinyume na taratibu
pia Katiba ya Nchi na kwamba, ziara hiyo imepangwa ili kuzindua wananchi wajibu
wa kudai viongozi waongoze kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.
Ziara
hiyo imepangwa kuanza kutekelezwa tarehe 7 Juni mwaka huu. Ziara hiyo itaanzia
mkoani Shinyanga, Wilaya ya Kahama.
Baada
ya hapo kutakuwa na timu mbili zitakazozunguka katika mikoa yote nchini ikiwemo
ya Chato, Bukoba, Geita, Sengerema, Muleba, Meatu, Bunda, Bariadi na kumalizika
Mwanza ambapo timu hizo mbili zitakutana.
Akizungumza
na waandishi leo Jijini Dar es Salaam Mkurungenzi wa Oganezesheni na Mafunzo wa
CHADEMA, Kigaila Benson amesema, timu hizo mbili pia zitafika katika nyanda zote
nchini zikiongozwa na viongozi wote wa chama pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya
chama na kisha ziara hiyo kumalizikia Dar es Salaam.
Benson
amesema, kwa kuwa Chadema ni chama kikubwa cha upinzani kina haki ya kufanya
ziara hiyo ya kuwafumbua macho na kuwaelimisha wananchi juu ya uongozi anaodai
wa kidikteta unaofanywa na Rais Magufuli.
“Tangu
kuingia madarakani Rais Magufuli kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na katiba,
serikali imekuwa ya mtu mmoja na maamuzi ya mtu mmoja kana kwamba, hakuna
wizara husika kitu ambacho kinawakandamiza wananchi na kushindwa kupata haki
zao,” amesema.
“Hatuta
choka kupiga kelele anapoenda kinyume na kupuuza Katiba ya nchi na tunataka
wananchi wa mtambue na wajue namna ya kudai haki zao. Tangu kuingia kwake
madarakani hakuna maendeleo zaidi ya kulipiza visasi kwa watu ambao
hawakumuunga mkono wakati wa kampeni.
“Rais
Magufuli amevunja na kuvuruga vitu vingi vilivyopo kwenye Katiba ikiwepo
sikukuu, kupanga matumizi ya fedha wakati wizara husika zipo, uvurugaji wa
bunge na mengine mengi yasiyomuhusu,” amesema.
Aidha
Benson amesema kuwa, wananchi nchini wajiandae kupewa elimu ya utambuzi na
kuanza kuchukua hatua juu ya utendaji wa mtu waliyempa dhamana ya kuwaongoza.
Pia amesema tayari wameshatoa taarifa katika vyombo vya usalama na hivyo
wananchi wasiwe na shaka

No comments
Post a Comment