WANAFUNZI WALIOFUKUZWA UDOM WAMJIBU RAIS MAGUFULI,WAIBUKA NA KUJIBU HOJA YA "VILAZA"SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli
kutangaza kuwa wanafunzi 7802 waliofukuzwa kwenye chuo kikuu cha Dodoma kuwa ni
“vilaza” na hawana sifa za kuwepo chuoni hapo huku akitakiwa kujiunga kwenye vyuo vyenye hadhi
yao.
Hatimaye nao wanafunzi hao wameibuka na kusema
wanasifa stahiki za kuwepo chuoni hapo,kutokana na kukidhi sifa ziliotangazwa
na serikali kwa wanafunzi ambao wanatakiwa kusoma chuo hicho.
Akizungumza na Waaandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam
kwa niaba ya wanafunzi hao,Ibrahim Abdallah amesema wao wanasikitishwa na kauli
ya Rais Magufuli kwa kusema Rais atakuwa anapotoshwa juu ya suala hilo kutokana
na wanafunzi wote waliopo hapo wanasifa ambazo zilitangwana Serikali.
Amesema sifa za udahili kwa wahitumu wa kidato cha
nne tu ambao wametapa daraja la 1,2 na 3 huku akitakiwa amefahulu kwa alama A
au B kwenye kwa masomo ya Sayansi.
Amesema licha ya serikali kutoa sifa hizo pia bado
walitoa nafasi kwa hata wanafunzi wa kidato cha nne ambao walipata darala la
nne ambao wao walitakiwa kusoma kozi maalum ya Cheti kabla ya kujiunga na ngazi
Stashahada katika chuo hicho.
Hata hivyo,Mwanafunzi huyo aliendelea kueleza kwa
uchungu amesema wanasikitishwa na hatua ya kukatishwa masomo yao huku bado
wanafunzi wengine ambao walikuwa wanatakiwa kumaliza masomo yao ndani ya mwezi huu sita jambo analodai hawana pakwenda kutokana na ndoto
yao yote ikiwa imepotea.
Hatahivyo,amesema hata kama Rais Magufuli ameona
mfumo huo wa kuwasomesha wanafunzi wa masomo ya Sayansi ulikuwa hauna tija,angetakiwa
kuuangalia jisni gani ya kuweza kuwasaidia wanafunzi kuriko hatua
iliyochukuliwa na kuwafukuza wote wanafunzi hao.,
Ameleeleza kuwa hata hoja ya Rais anayodai kuwa kuna
watoto wa Vigogo waliofeli ambao wamepenyezwa katika chuo hapo,wamesema
anatakiwa kuwashughulikia watendaji waliohusika kuwapitisha wanafunzi hao
kuriko kuishia kuwahusishwa wanafunzi wote huku akidai wengi wa wanafunzi hao
ni masikini.
Katika Hatua nyingine wanafunzi hao wamemuomba Rais
Magufuli kuangalia kwani wengi wao wanatoka kwenye Familia masikini.
1 comment
Vilaza ni vilaza tu, kutoka familia masikini hakumfanyi mwanafunzi kilaza akawa bora darasani, tunamuunga mkono mh.Rais wanafunzi wa aina hii wote OUT
Post a Comment