WAZIRI KAIRUKI AWAKOMALIA WATUMISHI WA UMMA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Angela Kairuki amewapa wiki moja waajiri wa sekta za umma nchini kukamilisha na kuwasilisha taarifa kuhusu watumishi hewa.
Bibi Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa za awali juu ya watumishi hewa zilizowasilishwa na Wakuu wa Mikoa nchini.
Amesema kuwa taarifa za Machi 1 hadi April 4 mwaka huu zinaonyesha watumishi 4,317 waliondolewa
katika Payroll ya Serikali ikiwa ni kasi ya kuondoa watumishi ambao
utumishi wao umekoma kwa kipindi kifupi ambapo haijawahi kufikiwa kwa
kipindi cha nyuma ikiwa ni mwitikio wa agizo la Rais Dkt Magufuli.
"Kutokana
na Mfumo wa HCMIS ambao hufungwa kila tarehe 5 ya kila mwezi umewezesha
Watumishi wa Serikali 1,284 kufutwa kwa Aprili 1 hadi 4 ikiwa
imejumuishwa watumishi hewa, waliostaafu, walioacha kazi waliofukuzwa na
waliofariki dunia"Amesema Angela.
Angela
amesema kuwa muda wa kufunga Payroll umeongezwa na utafungwa Aprili 12
ili kuhakiki watumishi wote wa serikali ambao hawastahili kuwepo kwenye
Payroll"
Pia
amesema kuwa baada ya tarehe hiyo Ofisi yake itafanya ukaguzi kwenye
taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha wale ambao
hawawajibiki au kutimiza wajibu wao katika eneo la usimamizi wa
rasilimali watu wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria
Hakuna maoni
Chapisha Maoni