WALIOTUMBULIWA MAJIBU SASA KUFIKISHWA MAHAKAMANI MDA WOWOTE,KATIBU MKUU KIONGOZI ASEMA UCHUNGUZI UNAKARIBIA KUMALIZIKA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI imesema ipo katika hatua ya mwisho kuhakikisha
wanakamilisha ushahidi kwa wale watumishi mbali mbali wa Umma waliosimamishwa
kazi kwa dhana ya “utumbuaji majibu” ili wafikishwe mahakamani.
Hayo yamemwa leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu
Kiongozi,Eng John Kijazi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa watendaji
wakuu wa taasisi na mashirika ya umma,ambapo amesema kwa serikali imeunda
kamati mbali mbali za uchunguzi kuwachunguza watumishi hao waliosimamishwa ili
wakamilishe ushahidi na kuwafikisha mahakamani.
‘Zipo kamati mbali mbali zinafanya uchunguzi, maana
ni wengi na kila kamati inafanya uchunguzi wake na uchunguzi ukikamilika na
tukijilidhisha kama baadhi wanamakosa ya kisheria basi hatua zitachukuliwa,nawakikishieni
ni baada ya mda mfupi tu uchunguzi unakamalika”amesema Eng,Kijazi.
Hata Hivyo,Eng Kijazi pia amezihatadhalisha idara
mbali mbali za serikali ambazo watumishi
wake hawajawasilisha taarifa zake za maadili basi idara hizo na watumishi hao
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria”
“Kamishna wa Kazi akituambia kama kuna baadhi ya
taasisi ya serikali ambazo watumishi wake wamekaidi kuleta taarifa zao za
maadili basi,tutawachukuliwe hatua kali,maana watakuwa wametenda kosa kinyume
na maadili ya utumishi wa umma na adhabu yake zipo nyingi”amesema Eng Kijazi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni