Zinazobamba

TRA YAZIDI VUNJA REKODI YA MAPATO NCHINI,YATIA FORA KWA MWENZI MACHI,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam


MAMLAKA  ya Mapato nchini (TRA) imezidi vunja rekodi ya ukusanyani wa mapato baada ya kukusanya mapato ya zaidi ya trioni 1.316 ambayo ni sawa na asilimia 101.0 kwa mwezi Machi ikiwa ni kiwango kikubwa tofauti na malengo waliyojiwekea ya kukusanya trioni 1.302 kwa mwezi huo.Anaaandika KAROLI VINSEN endelea nayo
 
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna mkuu wa TRA,Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema hali ya ukusanyaji wa kodi nchini inaendelea vizuri kwa madai kuwa TRA inavuka malengo ya ukusanyaji kodi waliyojiwekea.

“Tunazidi vunja rekidi ya ukusanyaji wa mapato kwani kwa mwezi Machi tulijiwekea malengo ya kukusanya Trioni 1.302 lakini baada kuweka mipango dhabiti tumejikuta tumekusanya Trioni 1.316 ambayo ni sawa na asilimia 101.0”amesema Kidata.

Kidata, ametoa sababu zilizopelekea TRA kuzidisha kiwango hicho cha ukusanyaji wa kodi imetokana na kuongezeka kwa kasi ya usimamizi,ufuatiliaji na ukadiriaji wa kodi kwa usahihi na bila uonevu pamoja na kudhibiti biashara za magendo katika maeneo ya ukanda wa Pwani wa bahari ya  Hindi pamoja na mipaka yote ya nchi.

Pamoja na hayo,Kidata ametoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini ambao hawajasajili biashara zao kufanya hivyo mara moja kupitia ofisi za TRA zilizopo katika maeneo yao.


Katika Hatua nyengine,TRA imesema inajaandaa kutoa mashine za kielekroniki za Kodi (EFDs) bure kwa wafanyabiashara nchini ikiwa ni kutii agizo la Rais John Magufuli aliitoa kwa Mamlaka hiyo kutoa mashine hizo bure.

No comments