Zinazobamba

WAZIRI MWIJAGE AJITOSA KUVIOKOA VIWANDA VYA NDANI,SASA KUTUNGA SHERIA,SOMA HAPO KUJUA






 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Nondo cha Kamal Steels Ltd. kilichopo Chang'ombe, DSM, pembeni yake ni Gagan Gupta ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji wa Kiwanda hicho.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akiangalia makopo yanayotumiwa na Kiwanda cha Kamal kama nalighafi za kiwanda akiwa na uongozi wa kiwanda.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akimuangalia fundi wa kusawazisha chuma kwa kutumia Shaper Mashine.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akipanda Mti wa kumbukumbu mara baada ya kukitembelea Kiwanda cha Kamal.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kamal wakishuhudia ziara ya Waziri kiwandani hapo




NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage amesema Serikali ipo mbioni kutunga ya sheria inatakayozuia uingizaji wa bidhaa zenye bei nafuu kutoka nje ya nchi ili kuvikuza viwanda vya ndani ya nchi,

Hata hivyo,Waziri Mwijage  amelitaka Shirika la Viwango nchini (TBS) kutoa miezi minne kwa wafanyabiashara wote ambao wanaingiza mafuta ya kurainisha mashine  kutoka nje ya nchi kuanza kuomba vibali TBS kabla ya kuingiza nchini ili kuzuia bidhaa feki,

Waziri Mwijage ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam,Wakati alipokuwa amefanya ziara kwenye viwanda vinne vilivyopo Wilaya ya Temeke Jijini hapa kwa lengo kuangalia uzarishaji kwenye Viwanda hivyo, kati yake kimoja ni kiwanda cha Nondo viwili ni vya kuzarisha mafuta ya kurainishia mashine na kimoja ni cha uuzaji wa Gesi za majumbani,

Ambazo Waziri Mwijage amesema kukamilika kwa sheria itakayozuia uingizaji wa bidhaa kutoka nje zenye bei ya chini kutavikuza viwanda vya ndani.

“Leo nimekuja kwenye kiwanda hichi cha Kamal steels Ltd tumeshuhudia jinsi gani Nondo zilivyojaa hapa kiwandani zimekosa mauzo kutoka na uingizaji wa nondo kutoka nje ambazo zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya nchini kuriko hizi na kupelekea kiwanda hichi kukosa masoko,”

“Na serikali haitaweza kuvumilia kuona viwanda vilivyopo nchini vinakufa kutokana na uingizaji huu,sasa nitahakikisha sheria inatungwa ambayo itakayozuia uingizaji huu wa bidhaa”amesema Waziri Mwijage,

Naye John Mekalemwene ambaye ni Fundi mkuu wa kiwanda cha Jamal Steel Ldt ambaye aliongea kwa niaba ya Uongozi wa kiwanda hicho amlimlalamikia Waziri juu  kukosekana kwa masoko ya bidhaa za Nondo kiwandani hapo ambapo amedai kuwa tatizo hilo limechangiwa na uingizaji wa Nondo kutoka nje.

Hata Hivyo Waziri Mwijage alitumia nafasi hiyo kuitaka TBS kutoa miezi minne kwa wafanya Biashara wote ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kuingiza mafuta ya kurainisha mashine kuanza kuchukuwa kibali  TBS kabla ya kuingiza mafuta hayo nchini,

“Viwanda vinavyozarisha mafuta ya kutainishia mitambo vinakosa soko nchini kutokana na uingizaji huu wa mafuta kutoka nje ya nchi,hii nawaomba TBS kutoa miezi minne kwa wafanyabiashara wote kuanza kuchukua kibari ndio waingize mafuta haya,kama mtu hana basi hasileta mafuta hapa,”amesema Waziri Mwijage,

Vilevile,Waziri Mwijaka alitumia nafasi hiyo kuwataka wafanyakazi wote wa viwanda ambavyo alivitembelea kuacha kulalamikia mishahara midogo wanayopewa na waajiri wao bali amewataka kuzidisha ufanyaji kazi kwanza na baadaye ndio waanze kudai nyongeza ya mishahara.

No comments