TAMWA YAENDESHA MAFUNZO JINSI YA KUTOA HUDUMA KWA WAHANGA WA UKATILI UNAOTOKANA NA UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na IOGT-NTO-Movement imeendesha mafunzo ya siku moja kwa wadau kutoka kata za Salanga, Makumbusho na wazo wakilenga kutoa elimu juu ya kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaotokana na unywaji wa pombe kupita kiasi
Mafunzo hayo yamelenga kuelekeza jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi.
Mkutano uliofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga ambaye ameitaka jamii kuchukua hatua ikiwemo kuachana na unywaji wa pombe kupita kiasi kwani ni hatari kwa afya zao na jamii kwa ujumla.
Mkutano huo pia uliwakutanisha wadau wengine wa madawati ya kijinsia, Viongozi wa dini na viongozi wa Serikali ya mitaa na Kata pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari.
Aidha, mambo mbalimbali yamejadiliwa katika mkutano ambapo imeelezwa kuwa katika Kata ya Saranga na maeneo ya Mbezi matatizo makubwa yanayoripotiwa ni pamoja na masuala ya ubakaji wa watoto na vitendo vya kulawitiwa ambapo asilimia kubwa vimehusishwa na pombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga akifungua mkutano huo wa siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akifungua mkutano huo kwa kusoma hotuba fupi ya namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi (Hayupo pichani)


Mkutano ukiendelea

Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo

Baadhi wanahabari washiriki katika mkutano huo

Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo

Baadhi ya washiriki kutoka katika maeneo ya jamii wakiwa katika mkutano huo

Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo.


Washiriki hao katika mkutano huo


Ofisa wa TAMWA katika dawati la Jamii na Jinsia, Bi. Marcela Lungu akitoa mada namna ya madawati ya kijinsia na namna ya kumpokea mteja na namna ya kulitatua.
Baadhi ya wakuu wa madawati ya jinsia pamoja na viongozi wa TAMWA

Mkurugenzi wa TAMWA akisalimiana na wadau washiriki wa mkutano huo ambao ni wawakilishi wa wananchi

Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa siku moja wa namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

No comments
Post a Comment