Zinazobamba

WAZIRI WA MAGUFULI ATUMBUA MAJIPU BANDARINI,AWAONDOA VIGOGO,SOMA HAPO KUJUA

Waziri Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa amewahamisha kazi watendaji  wa juu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) baada kuisababishia serikali hasara kwenye upotevu wa makontena katika bandari hiyo.
     Watendaji hao waliohamishwa kazi ni,  Piter gawilo ambaye alikuwa  mkurugenzi wa Rasilimali watu  ndani ya Mamlaka hiyo,ambaye ameondolewa kwenye nafasi hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Antony Mbilinyi ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa Rasilimali watu ndani ya Mamlaka ya Mawasiliano  nchini (TCRA).
    Wengine ni waliomishwa  Kazi ni Kaimu mkurugenzi  wa manunuzi wa TPA, Mashaka Kishanda ambaye nafasi yake nafasi yake imechukuliwa Benito Kalinga ambaye  awali alikuwa mtumishi wizarani hapo,
   Sanjari hao, mwengine aliohamishwa ni Kaimu mkurugenzi wa TEHEMA wa TPA,Kalian Charles naye nafasi yake imechuliwa  Abdullhaman Bamba ambaye awali naye pia walikuwa wizarani ya ujenzi.
   Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri Mbarawa amesema nia ya serikali ya kuwaondoa watendaji hao ni kukata kuongoza kasi ya ukusanyaji mapato ndani ya TPA.
  “Serikali imefuikia uaamuzi huu,kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji kodi kwenye Mamlaka ya Bandari ndio maana tumewaondoa watendaji hawa tumewaweka watu ambao watazidisha kasi ya ukusanyaji mapato “amesema Waziri Mbarawa.
Hata hivyo,Waziri Mbarawa amesema watendaji hao waliondolewa kwenye nafasi hizo,wamerejeshwa wizarani na kusubuli kupangiwa kazi nyengine.

Hakuna maoni