Zinazobamba

MAGUFULI ACHARUKA AIFUNGIA KAMPUNI YA SIMU,PIA AZIFUNGIA REDIO 28 NCHINI,SOMA HAPO KUJUA

Pichani wa kati kati ni Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Masiliona,Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa

NA KAROLI VINSENT
SERIKALI nchini imetangaza kuifungia kampuni ya simu ya six Telecom pamoja na kuifungulia jarada la kiuchunguzi polisi, baada kubainika kuwa ilikosesha serikali mapato yaliyotokana na kodi yanayofikia bilioni 8.5 pamoja na kutoza gharama ya simu kwa  wateja  kwa kiwango cha chini tofauti na ile iliyopangwa na serikali.
    Hata hivyo,Serikali pia imetangaza kuzifungia redio 28 nchini baada ya kushindwa kulipia ada ya reseni.
   Akitangaza uaamuzi huo,leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa  amesema serikali imefikia uamuzi wa kuifungia  Kampuni hiyo ya simu baada ya kufanya makosa mbali mbali,
    Waziri Mbarawa ameyataja makosa hayo kuwa  ni kuikosesha mapato serikali yaliofikia billion 7.2 na  kukataa kulipa ada ya reseni ambayo ni bilioni 1,pamoja na kugoma kulipa toza ya faini ya milioni 361.25
   “Kwaanzia sasa tumeifungia kampuni hii ya Six Telecom baada ya kukiuka sheria mbalimbali ambapo Kampuni hii ya simu ilisajiliwa kutoa huduma  mwaka 2013,lakini ikaanza kukiuka kanuni  za Mamlaka ya mawasilioni nchini (TCRA) ambayo iliweka kiwango cha chini  cha gharama kwa kupiga simu nje ya nchi wakati ilitakiwa kutoza gharama kubwa,”
 “Licha kutoza kiwango  hiki cha  chini ya  kiwango pia imeshindwa kulipa kodi  ya Bilioni 7.2  pamoja na kukataa kulipa  gharama za reseni inayofikia bilioni 1 na kushindwa  kulipa faini ya milioni 361.25 iliyotokana kukiuka  kanuni za huduma hiyo”amesema Mbarawa.
   Vilevile,Waziri Mbarawa ametangaza kuzifungia rasmi redio 28 nchini baada ya kushindwa kulipa  ada ya reseni  kwenye Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA jambo analodai  kuwa ni kosa.
“Tumezifungia redio 28 ambazo Kesho (TCRA) watazitaja kwa majina,kwani redio hizi zimeshindwa kulipa ada ya reseni ambapo kisheria wanatakiwa kulipa,lakini redio hizi zilishindwa kulipa ”amesema Waziri Mbarawa

Hakuna maoni