WAISLAM NCHINI WANYOSHEWA KIDOLE ,NI KUHUSU VURUGU,SHEKH JALALA AENDELEA KUWAHASA,SOMA HAPO KUJUA
WAISLAM
nchini wamehaswa kutunza amani ya nchi kwa kuendelea kufanya mambo mema na
kuacha kufanya mambo ya kuchochea vurugu katika jamii.Aaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Wito
huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam, na mwenyeki wa Taasisi ya Kislam ya imamu Bukhari Foundation. shekh Khalifa
Khamisi wakati wa semina iliyowakutanisha waumini wa dini hiyo jijini
hapa,yenye lengo la kujadili Changomoto
zinazowakabili waislam nchini na Duniani kwa ujumla.
Ambapo
Shekh Khamis amesema kwa sasa waislam wamekuwa wanafanya mambo ya kumkera
mwenyezi mungu kwa kuwafanyia wenzao mambo ya maovu jambo analodai aliendani na
mafundisho ya Dini hiyo.
Waumini mbalimbali wa dini ya Kiislam kutoka maeneo tofauti wakisikiliza mafunzo kutoka kwenye semina hiyo.
Amesema
katika mafundisho ya dini hiyo,yanawafundisha waislam kuwa na upendo kwa jamii,kusaidiana
pamoja na kuelekezana na kufanya mambo ya maendeleo.
Amefafanua
kuwa kwa sasa watu wengi wamekuwa wakihusiha
masuala ya ugaidi yanayotokea Duniani na Dini hiyo,jambo analipinga kwa
kusema watu wanaofanya vitendo hivyo sio waislam safi kwani dini hiyo
afungamani na mambo ya Ugaidi.
Hata
Hivyo Shekh Khamis amesema kwa sasa
nchini kumekuwa na mgawanyiko kati ya Waumini wa dini ya Kiislam na
Serikali ambapo amedai sababu hiyo imetokana na hatua ya serikali kuwakamata
viongozi wa dini hiyo.
“Katika
semina hii tumekutana na waumini wa dini hii,ili kurudusha upendo katika jamii
ya waislam nchini na serikali,maana baadhi ya waislam waliiwekea chuki serikali
na leo tumetumia nafasi hiyo kuwataka waislam nchini kuondoa na hali hii na
kuichia vyombo vya mahakama ndio vitatenda haki”amesema Shekh Khamis.
pichani ni Shekh Hemed Jalala akiongea na wanahabari
Kwa
upande wake Shekh Hemed Jalala ambaye naye alikuwa mchangia mada katika semena
hiyo,amehasa pia Waislam kuendeleza kufanya mambo mema yatakayomfurahisha Mtume
Muhamed kwa kusema ndio njia pekee ya kuendana na dini hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni