VIGOGO WA NEMC YAWAKUTA NAO,SOMA HAPO KUJUA
VIGOGO NEMC WASIMAMISHWA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA
MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC
Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:
1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya
punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na
wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda
hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe
kazi mara moja:
a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja
la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa
Mazingira
Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia
2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa
watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu
utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya
apewe barua ya onyo kalian la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi
wa Baraza.
3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu
la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na
majukumu yaliyoko kwenye Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe.
Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili
kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa
hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.
4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa
NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo:
Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp
ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na
watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara
moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.
5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika
utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC
ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta
wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao
likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha
kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji
wa maombi yao.
6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa
Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika
Baraza.
IMETOLEWA NA
IDARA YA MAZINGIRA,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TAREHE 24.01.2016
Hakuna maoni
Chapisha Maoni