Zinazobamba

TAASISI YA KARIMJEE YATOA TUZO ZA WANASAYANSI CHIPUKIZI,SOMA HAPO KUJUA


pichani ni washindi wa jumla wa tuzo za wanasayansi chipukizi za young Scientinsts wakikabidhiwa vyeti

NA KAROLI VINSENT
KATIKA kuinua sekta ya sayansi nchini,Taasisi ya Karimjee Jinavanje imewatunuku nafasi za masomo Edmound Luguku na John Method  wanafunzi wa shule ya sekondari ya mzembe  kuwa washindi  wa jumla ya tuzo za wanasayansi chipukizi za Young Scientinsts Tanzania kwa mwaka 2015.
Hayo yametokea leo jijini Dar es Salaam wakati wa halfa fupi ya kuwaaga  washindi hao,ambapo akiongea na wanahabari wakati wa halfa hiyo,Meneja wa taasisi hiyo,Devotha Rubuma amesema washindi hao wawili walipata fursa  ya kupelekwa masomoni baada ya kumaliza kidato cha sita.
Ameeleza kuwa washindi watasafiri leo kuelekea Dubiln nchini Ireland ambapo watahudhuria maonesho  ya kimataifa ya sayansi na Teknolojia  ambapo  kila mwaka  hufanya mashindano yanayolenga kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupenda sayansi,


Kwa upande wake mwenyekiti wa heshima ya kundi la makampuni ya KarimjeeJivanje,Hatim Karijee amesema tuzo lengo la shindani hilo ni kutoa uwezo kwa watanzania,
“Tumepewa heshima kubwa sana kuweza kuwa sehemu ya tuzo za Young Scientist Tanzania kwani tunaamini kwamba elimu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania na pia kwa sababu elimu ya sayansi inaweza kuleta  fursa nzuri kitaalum”amesmea Karimjee.
Karimjee ameongeza kuwa  lengo la kimtazamo wa taasisi hiyo hivi sasa  ni kuisadia taasisi za elimu kwa kuboresha uwezo wake,familia ya karimjee ilianisha taasis mbali mbali za misaada kwenye  miaka  ya 1950 kabla ya uhuru.
“Tumejenga shule nyingi ,hospitali ,zahanati na vituo vya huduma za kijamii ambazo  mojawapo ya misaada wetu mkubwa ni ukumbi wa mkubwa wa Karimjee  ambazo tuliujenga  ambao  tulilenga na kuutoa  msaada kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1957”

Hakuna maoni