Zinazobamba

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAUMBUA MWAKYEMBE NA SITTA,SASA HATMA YAO IPO MIKONONI MWA MAGUFULI,SOMA HAPO


HATUA  inayochukuliwa na Waziri mkuu,Kassim Majaliwa ya kubaini ubadilifu mkubwa fedha  ndani ya Bandari ya Dar es Salaam na upotevu wa Bilioni 12 kwenye Shirika la Reli ya kati nchini TRL kunawazidi “wavuo nguo” Mawaziri wandamizi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.Mtandao huu unaripoti anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

     Mawaziri hao ni Samwel Sitta na Dkt Harrison Mwakyembe ambao wote walikuwa wanaongoza wizara ya Uchukuzi kwa nyakati tofauti kabla ya  mmoja wao kuhamishwa kwenye wizara tofauti na uchukuzi.

    Washirika hao ambao mara kwa mara wamekuwa wakijiapiza na kutaka kujiaminisha kwa umma kwamba ni watu waadilifu na wasimamizi wazuri wa mali za umma,sasa hali hiyo imefutika kabisa kwenye macho ya jamii.

        Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Serikali pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM ambazo mtandao huu umezipata zinasema hatua inayochukuliwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa ndani bandari hiyo ya kubaini upotevu wa Kantena zaidi ya 2000 kunazidi waweka msalabani mawaziri hao kwakuonyesha ni kama walishinda kuisimamia bandari hiyo au wao kuhusika katika kubaliki wizi huo.

     “Ninachokuambia Mwandishi (Mwakyembe na Sitta)hawana jipya kwa jamii yaani Majaliwa alichokifanya Bandarini ni ishara tosha ya watu hawa kujiuliza mara mbili walikuwa wanafanya nini uchukuzi wizara hii inasimamia Bandari na TRL,wameshindwa hata kuzuia wizi huu,”

     “Yaani uwezi ukatenganisha wizi wa Bandarini bila hata kuihusisha wizara ya uchukuzi ambayo kipindi cha Makontena hayo yanapotea kwaanzi mwaka 2014 hadi 2015 wizara ya uchukuzi ziliongozwa na Sitta na Mwakyembe jiulize waliokuwa wap?,endapo Rais Magufuli akisema achukue hatua zaidi hapo Lazima Mwakyembe na Sitta watafikishwa mahakamani”amesema matoa taarifa wetu aliyoko ndani yaSerikali.

        Kuhusishwa huku kwa Wanaojiita na kuitwa wapambanaji wa Ufisadi Mwakyembe na Sitta kunakuja ikiwa ni tayari hatma ya madudu yao ikiwa ipo mikononi mwa Rais Magufuli kutokana na kuhusika kwenye madudu mengine,

      Madudu hayo mengini yanawagusa ni kila moja wao  wanatuhumiwa kuhusika au kunyamazia ununuzi wa mabehewa mabovu ambayo yameitia hasara serikali ya zaidi ya Mabilioni ya fedha,

      Dkt Mwakyembe anatuhumiwa pia kuhusika au kuwanyamazia Wakurungenzi wa TRL pamoja na wa Wizara ya Uchukuzi kwa kuhusika kununua mabehewa ya Mizigo mabovu 256  ambayo yanatajwa kuwa  yalioitia hasara serikali ya bilioni 230,

     Huku naye Sitta akituhumiwa kuhusika kwake au kuwafumbia macho viongozi wa uchukuzi na TRL mpaka kuhusika kwao kununuliwa kwa Mabehewa ya kubebea mafuta ambayo yamegundulika wiki iliyopita kuwa nayo ni mabovu,

       Ugunduzi wa Mabehewa hayo yanahisiwa moja kwa moja ni mabovu yaligundulika wiki iliyopia mara baada ya Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi,Dkt Shaaban Mwinjaka kufanya ziara kushtukiza ndani ya shirika la TRL na kubaini kati ya Mabehewa 50  mapya yalionunuliwa yalipojaribiwa tu kwa mara ya kwanza yamebainiaka matano kuwa ni mabovu baada ya kuanguka njiani 
jambo analosema  Dk Mwinjaka kuwa endapo wangefanya majaribio mara tatu basi uwenda mabehewa yote yangeanguka.

          Akizungumzia hali hiyo,Mchambuzi wa siasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Jackson William amesema madudu yanaoyotokea Bandarini na TRL ni wazi Rais Magufuli anatakiwa kumburuza mahakani Sitta na Mwakyembe kutokana na kushindwa kusimamia wizara.

     “Kama kweli CCM wakiachana na mfumo wa kulindana ni wazi basi wanatakiwa kumchukulia hatua kali mawaziri hao ikiwemo kuwapandisha mahakamani haraka sana :

Hakuna maoni