Zinazobamba

VURUGU ZA DAR LEO KUHUSU BOMOA BOMOA,KOVA AWAJIA JUU WANANCHI ,SOMA HAPO KUJUA




NA KAROLI VINSENT
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewataka wananchi wa maeneo ambayo baraza la Mazingira,NEMC linapita likiweka alama ya ‘ X’ kwa ajili ya kubomolewa kuacha kuwafanyia fujo maofisa hao, lasivyo jeshi halitasita kumchukulia hatua kali mtu au watu watakao washambulia watendaji hao wa Nemc.
Kalipio hilo la jeshi la polisi linakuja ikiwa ni saa chache kupita baada ya wakazi wa maeneo ya Jangwani,Kigogo Jijini Dar es Salaam kujitokeza na kufunga barabara zote zipitazo maeneo hayo kwa kile wanachokidai kuwazuia maafisa wa NEMC wanaoweka alama ya X kwa ajili ya kuwakumbusha wakazi hao kujiiandaa kuhama kabla ya  wiki ijiyo bomoabomoa inatarajia kuaanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jioni hii ya leo Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Kanda Maalum,Suleiman Kova amesema Jeshi hilo limepokea kwa masikitiko kwa wananchi ambao ni wavunjaji wa sheria wanaowavamia maofisa wa NEMC kuwazuia kufanya kazi zao.
“Tumepata taarifa hizo,tukawatuma maaskari wameenda pale wamefanikiwa kuzuia fujo hizo,ila nawaambia wananchi waheshim sheria za nchi na utawala uliopo madarakani,nawahakikishia kuwa tutaweka ulinzi hadi siku ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo siku jumanne”amesema Kova.
Kova ameongeza kuwa kwa sasa ni lazima nyumba hizo zivunjwe kwani zimekiuka sheria ya ardhi,mazingira pamoja na mipango miji jambo analodai kuwa serikali hii itazivunja bila hata kumwogopa mtu.
Alipohitajika kuzungumzia zoezi hilo kwakuwa alikuwepo wakati tukio zima hadi kumalizika kwakwe, Heche aligoma kuzungumzia zoezi hilo kwa kudai kuwa mzungumzaji mkuu ni Waziri anayehusika na Mazingira, January Makamba au Mkurugenzi wa NEMC.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi waishio katika bonde hilo ni kutaka jengo la Stendi ya mabasi yaendayo haraka pia liwekewe alama na hatimaye kubomolewa kwa sababu ya kuwa jengo hilo lipo bondeni sawa na nyumba zao,

Aidha wameiomba serikali kuongeza siku zaidi za maandalizi ili waweze kuhamisha vitu vya majumbani kwani muda uliotolewa hautoshi kufanya maandalizi.

Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa nyumba zilizopo mabondeni lilianza Desemba 17 mwaka huu na kusitishwa baada ya siku tatu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5 kwa kigezo cha kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao .

Hakuna maoni