Zinazobamba

RUNGU LA MAGUFULI KUZIANGUKIA BAA,MAKANISA,VIWANDA,SASA KUFUNGWA RASMI,NEMC YASEMA KANUNI IMESHAPATIKANA,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Mkurugenzi wa NEMC mhandisi, Bonaventure Baya wakati akizungumza na waandishi wa habari

BARAZA la Uhifadhi na  Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limesema litazifunga Baa,Makanisa pamoja na Viwanda ambavyo vimekuwa vingifungilia sauti kubwa ambazo zinawakela wananchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hatua hiyo imetangazwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa NEMC mhandisi Bonaventure Baya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mara baada ya sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kupatikana kanuni zake ambazo kanuni hizo zinaruhusu rasmi kutimika kwa sheria hiyo,
Amesema sheria hiyo ya mwaka 2004 imetoa katazo kwa  mtu yeyote kusababisha kelele yenye kubughuzi,kudhuru,kuhatarisha faraja ya mtu mwengine.
Hata hivyo sheria hiyo imeweka adhabu kwa mtu atakayekaidi sheria hiyo na kuendelea na kupiga kelele kwa wananchi kwa kuanisha  adhabu kwa mahakama isiyopungua Tshas 50,000 na isiyozidi milioni 50,
Sanjari na faini hizo pia kanuni hiyo ya mazingira kifungo 194 (1) inatoa mamlaka kwa NEMC ku

fungia eneo au kuweka katazo kwa sehemu husika ambayo imekubuhu kwa kelele hizo,
Baya ameyataja maeneo ambayo yamekuwa yakilalamikiwana wananchi kukidhili kwa kelele ni Viwandani,baadhi ya makanisa,pamoja na viwandani,
Vilevile Baraza hilo limesema litahakikisha linashirikiana na sekta zote,wizara.Mamlaka za Serikali za miotaa na Halmashauri na Manispaa ya majiji pamoja na mamlaka zote za umma kwa ujumla lili kuzingatia na kuetekeleza kanuni hizo.

Hakuna maoni