Zinazobamba

DC MAKONDA APANIA KUMALIZA TATIZO LA UHABA WA SHULE ZA SEKONDARI,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda

KATIKA kukabiliana na tatizo la ukosefu wa shule za Sekondali za  kata katika manispaa ya Kinondoni,mkuu wa wilaya hiyo,Paul Makonda amesema amedhamilia kujenga shule hizo sita kuanzia Januari 5 hapo mwakani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
    Makonda ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa wilaya yake inatatizo la ukosefu wa shule hizo jambo analodai limechangia wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kujiinga na kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa shule hizo,
Ametole mfano matokeo ya darasa la saba ya mwaka

huu yanaonyesha wanafunzi 15,185 walipata nafasi ya kujiiunga na shule za sekondari katika chaguo la kwanza  lakini kati ya wanafunzi hao wanafunzi 3,183 licha kufahulu kwao wamekosa nafasi ya kujiiunga na kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa shule,
      Makonda ameyataja maeneo yaliokumbana na uhaba wa shule hizi ni  katika kata za Mzimuni,Ubungu,Kimara,Kinondoni,Magomeni na Mbezi juu,
      Amesema baada ya kubaini shida hizo amechukua hatua ikiwemo kushirikiana na wadau wa maendeleo walioko ndani ya wilaya yake hiyo kuhakikisha wanapata fedha za kuhakikisha wanaanza ujenzi wa shule hizo haraka sana.
  Ameongeza kuwa Ujenzi wa shule hizo utakwenda na kasi ya haraka ikiwemo kufanya kazi usiku na mchana katika ujenzi wake ili  kuhakikisha wanafunzi hao waliokosa kujiiunga kidato cha kwanza wanajiiunga haraka na kuanza masomo yao.

Hakuna maoni