Zinazobamba

PROFESA LIPUMBA AIBUKA TENA OFISI ZA CUF,SASA AMVAA RAIS SHEIN,SOMA HAPO KUJUA


????????????????????????????????????


NA KAROLI VINSENT
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Wananchi,CUF,Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kuacha kung’ang’ania madaraka, badala yake amemtaka kumwachia mgombea wa Urais wa CUF Maalim seif shaarif Hamad ambaye amedai ni mshindi halari,
  Hata hivyo, amesema  Dkt Shein akiendelea kukaidi basi atapelekea kutokea machafuko makubwa ambayo yaliwai kutokea visiwani Zanzibar mwaka 2001.
     Profesa Lipumba ambaye alijiuuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF miezi mitano iliyopita kutokana na kutokubaliana  aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Edward Lowassa ambaye chama cha CUF kilikuwa kinamuunga mkono,
      Ambapo Leo Profesa Lipumba ameibuka tena kwenye Makao mkuu ya CUF yalioko Buguruni Jijini Dar es salaam na kuzungumza na waandishi wa habari ambapo Amesema Dkt Shein anatakiwa kuachia madaraka kwa madai kuwa ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika.
‘Mimi namsihi Dkta shein aache ukaidi,ameshashindwa kwenye uchaguzi ule,akubali Mgombea wa CUF ambaye ameshinda kihalari aongoze maana anavyozidi kuendelea kung’ang’ania ataweza hata kuharibu amani na utulivu ulioko visiwani zanzibar na kuingiza Zanzibar kwenye machafuku kama ya mwaka 2001”amesema Profesa Lipumba.
      Amesema kuwa kitendo cha Dtk Shein kuendelea kubaki madarakani na kung’ang’ania uchaguzi urudiwe akikubaliki amedai kuwa  kunazidi ichafua Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwenye medani ya kimataifa.
    Ameeleza kuwa hatua iliyochukuliwa  shirika la Millennium Challenge Corporatinon-MCC kwa serikali ya Tanzania kuinyimwa msaada wa dola Milioni 698,kutokana na kile anachokiita ni “Ubabe” wa Dkt Shein kubaki madarakani kunazidi dharotesha uchumi wa Tanzania.
“Dkt Shein anachofanya cha kutokubali matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kutaathiri mahusiano yetu na nchi nyengine hasa jumuiya za ulaya,ajiuulize suala la msingi anataka kuleta machafuko ya kisiasa Zanzibar”ameongeza
Profesa Lipumba ambaye ni msomi wa uchumi amefafanua hasara ya kiuchumi ambazo Taifa litaweza kuzipata kutokana na mgogoro huo,kwa kudai kuwa   Tanzania  itafutwa kwenye mpango wa Rais wa Marekani Barack Obama wa kuisadia nchi katika kupata umeme katika kila vijiji,
“Huyu Shein anataka kumuhujumu Rais Obama asifanikishe mpango bwake wa power Afrika kabla hajang’atuka mwaka 2016?,alihoji Profesa Lipumba
Pamoja na hayo,Profesa Lipumba amemuomba Rais John Magufuli kuitaka tume ya uchaguzi Zanzibar,ZEC  kutangaza matokeo yaliyobaki ili nchi iweze kusonga mbele,

Hakuna maoni