TFDA YAKAMATA BIDHAA BANDIA,YAMO MAZIWA YA WATOTO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kupitia shirikisho la Kimataifa
limefanikiwa kuzikamata dawa ,vipodozi ,vinywaji pamoja na maziwa ya watoto
ambavyo ni Bandia vyenye thamani milioni 26.
Hata
hivyo pia wamefanikiwa kuzikama bidhaa ambazo hazisajriwa na mamlaka husika.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu oparesheni iliyojulikana “Fagia 1” ambapo Opareshini hiyo ilianza
Desemba 10 hadi 11, ,Mkurugenzi wa mkuu wa ( TFDA),Hiiti Sillo amesema ukaguzi
huo ambao ulifanyika katika maeneo 124 ya jijni dare s Salaam,
Ametaja
sehemu hizo ni maduka ya vyakula ni 29,baa 2,supermaekets 20.mini-supermaekets
27,maduka ya pombe/vinywaji vikali 6,ghala 1 pamoja na maduka mengine ya
vinywaji ya rejaeja 39.
Wanahabari wakimsikiliza mkurugenzi wa (TFDA) |
Sillo
amezitaja bidhaa hizo ambazo ni bandia zilizokamatwa ni Vyakula vya watoto kama
Maziwa ya Cerelac mixed vegetable,wheat with milk, pamoja na maziwa ya watoto
wachanga mbali mbali aina ya SMA,promil gold,
Sanjari na
Maziwa pia Sillo ametaja bidhaa zengini kinywaji cha Jack Daniel’s Whiskey na makopo 66 Royco mchuzi mix beef flavor,
Sillo
amebainisha kuwa maduka ambayo yamekutwa
na bidhaa hizo yamekiuka sheria ya chakula ya dawa na vipodozi sura 219,na kusema hatua mbali mbali za kisheria
zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni maduka hayo,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni