WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI HATARINI,TCRA KUZIFUNGA RASMI,OMBENI SEFUE NAYE APIGILIA MSUMARI WA MWISHO
Katibu mkuu kiongozi,Ombeni Sefue akizungumza na wanahabari pamoja na viongozi wa (TCRA) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa simu za mkononi leo makao makuu ya TCRA jijini Dar es salaam |
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa miezi
sita kwa watumiaji wa simu za mkononi
ambao wanatumia simu bandia kuachana nazo la sivyo watazifungia.
Pia TCRA imetoa mwongoza kwa watumiaji wa simu hizo
kuzihakiki simu zao kama ni harali, ambapo watumiaji wanatakiwa kupiga simu*#06# harafu zitatokea namba mara baada ya kupiha na kinachotakiwa ni kuzichukua namba hizo kisha kwenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi na
kuziandika namba hizo,
Harafu unatuma ujumbe wa namba hizo kwenda kwenye namba maalum 15090 na kutapata matokeo kamili kuhusu uhalali wa simu ikiwemo pia
kuzisajili.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa (TCRA) Dkt Ally Simba wakati akiutambulisha, mfumo mpya wa rajisi
ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, kwenye makao makuu ya Mamlaka hiyo
yaliopo Jijini Dar es salaam,ambapo amesema nia ya TCRA ni kuziondoa simu zote bandi
katika mfumo wa utumiaji wa simu.
Pia amesema mfumo huo utasaidia kuongeza usalama
mtandaoni kwa watumiaji wa simu kwa madai kuwa simu zote za mkononi zitakuwa zimejulikana kutokana na kusajiliwa kwenye
mfumo huo na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango hivyo kusaidia
kuepeka madhara yatokanayo na simu zisizokuwa bora stahiki.
Wadau wa simu za mkononi,watendaji wa TCRA pamoja na wanahabari wakimsikiliza Ombeni Sefue na Dkt Simba |
Sanjari
na hayo,Dkt Simba amesema mtumiaji wa simu atakuwa na uwezo wa kuripoti mara
simu yake inapoibiwa na kuifanya isiweze kutumika na mtandao wowote wa simu
hapa nchini na kupelekea kupungua wizi wa simu.
Kwa
upande wake Katibu mkuu kiongozi,Ombeni Sefue ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati
wa uzinduzi wa mfumo huo amewataka watanzania kuachana na tabia ya kutimia simu
kwa matumizi ya uharifu.
“Hatuwezi
kukubali kama serikali kukawa na watu wanatumia simu kwa matumizi ya kufanyia
uharifu kutapele watu,kwa kweli tumechoka sasa nauhakika mfumo huu utasaidia
kuwakamata watu hawa wanasumbua watanzania”amesema Sefue
Hakuna maoni
Chapisha Maoni