Zinazobamba

SERIKALI KUPATA HASARA TENA,MABEHEWA MABOVU YANGUNDULIKA,NI TOFAUTI NA YALE YA MWAKYEMBE,SOMA HAPO KUJUA

Pichani wa Katikati ni Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi,Dk Shaaban Mwinjaka alipofanya ziara ya kushtukizaKwenye shirika la reli ya Kati,TRL
NA KAROLI VINSENT
 WAKATI kukiwa bado  haijulikani hatma ya  Watendaji wa juu wa shirika la Reli ya kati TRL,  ambao walihusika kuitia hasara Serikali kwenye ununuzi wa Mabehewa  mabovu ya kubebea mizigo 250 ambayo yenye thaman ya Bilioni 200.
    Wizara ya Uchukuzi ambayo yenye dhamana na Mabehewa hayo imebaini tena mabehewa  mengine matano kati  50 ambayo yalinunuliwa kwa ajili ya kubebea mafuta kuwa yanakasoro.
    Ugunduzi wa Mabehewa hayo yanayodaiwa ni Mabovu yamegundulika Leo Jijini Dar es Salaam,mara baada ya Katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,DK shaaban Mwinjaka alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Shirika la Reli ya kati,(TRL) ambapo Katibu huyo alipofika hapo alimtaka Mkurugenzi wa TRL atoe ufafanuzi juu ya Mabehewa hayo.
       Mwinjaka alidai Mabehewa hayo ni mapya ila ameshangazwa kuwa wakati yalipokuwa yanafanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi yalipofika njiani Mabehewa matano kati ya 50 yakaanguka njiani.
     “Yaani aingii akilini kabisa yaani mabehewa ya treni haya tena ni mapya kabisa tumenunua tu juzi,leo nimesikia mmeyajaribu kwa kubeba maji yakaanguka njiani matano kwa safari moja moja tu je kama tungeenda  safari tano kwa tafsiri hiyo yangeaanguka mengi,”amehoji Mwinjaka.
    Mara baada ya Mwinjaka kuwabana wakurugenzi hao wa TRL ndipo wakakosa majibu juu ya Mabehewa hayo,baada ya hali hiyo ikamlazimu kuunda kamati itakayochunguza ubora wa Mabehewa hayo kujua kuwa ni mazima au la.
    “Sasa hapa ni kazi tu,nimeunda kamati ya wataalamu itakayochunguza  ubora wa Mabeheha hayo tujue kama ni mabovu basi hatua kali zichukuliwe kwa watu waliohusika katika ununuzi huo,ikiwemo tuwarudishia Kampuni iliyohusika na kuyatengeneza mabehewa haya”
         Kuibuka huku kwa sakata hili la Mabehewa mabovu ya kubebea mafuta kuna kuja ikiwa ni teyari serikali imeingia hasara za Bilioni 200 kwenye ununuzi wa mabehewa ya Mizigo yanayofikia 250,
         Ambapo kwa mujibu wa Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta aliunda kamati maalum uliyochunguza ubora wa mabehewa hayo na kubaini ni mabovu huku watendaji wa TRL wakihusika katika kukiuka kanuni ya manunuzi ya Umma yaliyowataka kuzingatia hatua zote.
        Sitta alisema viongizi hao wa TRL waliohusika na hali hiyo watafikishwa mahakamani,lakini jambo la kushangaza ni takribani mienzi mitano imepita hakuna hata mkurugenzi mmoja alifikishwa Mahakamani.
        Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti zilisema kitendo cha Rais Mstaafu,Jakaya Kikwete kumuundoa aliyekuwa mtangulizi wa Wizara ya Uchukuzi,Harrison Mwakyembe na kumpeleka Wizara ya Afrika Mashariki ilitajwa ni kumwokoa kwenye Kashfa hiyo,

Katika Hatua Nyengine Katibu Mkuu huyo amelita Shirika la TRL kuhakikisha wanashirikiana na wadao wengine wa Reli ili wakifufue kiwanda cha kutengeneza Bleki za treni na kuacha Tabia ya kuagiza Bleki hizo nje ya nchi.  

Hakuna maoni