ZITTO KABWE AIAMSHA IKULU YA MAGUFULI,SASA BENK YA STANBINK YAINGIA MATATANI TENA,SOMA HAPO KUJUA
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. |
NA KAROLI VINSENT
BENKI ya Stanbink iliyokuwa inatumika kuchota pesa
na watuhumiwa wa Ufisadi kwenye sakata
la Akaunt ya Tegeta Escrow iliyokuwa ndani ya Benki kuu ya Tanzania,B.OT,sasa Benki hiyo imeingia matatani tena
baada ya Ikulu kuibuka na kuitaka kuilipa serikali ya Tanzania fidia,
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza
na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tuhuma
zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya
udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 iliyopewa serikali ya Tanzania na
Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.
Kashfa hiyo ambayo iliibuliwa na
Mbunge wa Kigoma Mijini kupitia Chama cha ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe jana
kupitia kwenye Vyombo vya Habari ambapo aliitaka serikali kuingilia kati,
Ambapo Sefue amesema kuwa
Benki kuu ilifanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo
yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma,malipo
hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki
hiyo walishindwa kuvumilia kwa hiyo tetesi tukazipata, wakaguzi wa benki kuu
walifuatilia,
malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi
wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu
zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa
kwenye kampuni ya Kampuni ya Egmwa na siku chache zilitolewa zote kwa fedha
taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya
kodi ilipaswa kutozwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni