Zinazobamba

NHIF YAJA NA KITU BORA KWA WATANZANIA,SASA YAENDANA NA KASI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz na mawasiliano kwa njia ya mtandao (Mitandao ya kijamii na simu za mkononi), uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.Picha na Michuzi Blog
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ya NHIF, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akionyesha kipeperushi chenye namba ya mawasiliano ya moja kwa moja na kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SoftNet Tech, Nuru Yakub Othman wakishirikiana kuzindua rasmi Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kushoto) akimuangalia Ofisa Uanachama wa Kituo cha Mawasiliani ya Huduma kwa wateja, Eva Mkwizu wakati akiwasiliana na wateja wa njia ya simu. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba
Baadhi ya Maofisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiendelea kutoa huduma katika kituo hicho.
sab1Mmoja wa Maofisa wa mfuko huo Sabina akiendelea na kazi yake.




Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umezindua rasmi leo Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz

Kituo hicho cha mawasiliano kitakuwa na jukumu kubwa la kuunganisha Mfuko na wadau wake, wakiwemo wanachama, watoa huduma na wananchi kwa ujumla. Kitakuwa ni mahali pa kwanza pa kupata taarifa na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na huduma za Mfuko, hivyo kuondoa au kupunguza ulazima wa wanachama au watoa huduma kufunga safari hadi kwenye ofisi zetu ili kufuata huduma ambazo zingeweza kupatikana kwa urahisi kwa njia ya simu au ujumbe wa maandishi.

Mfuko umekuwa ukiboresha njia za kuwasiliana na wadau wake ili kuweza kufikia dhima yake ya kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wanachama wake na wadau kwa ujumla.
Ni wito wa NHIF kwa wadau wote nchini popote walipo waweze kutumia namba hii 0800 110063 kwa mawasiliano yoyote na Mfuko ili tuweze kushughulikia hoja, maswali yao na pia kutupatia mrejesho wa huduma wanazopata za NHIF. Nasi kwa upande wetu tunaahidi kutumia kituo hiki vema kuboresha huduma zetu kwa wadau.  

Maoni 1

Unknown alisema ...

Naomba kuuliza, mimi na mme wangu tumestaafu na tulikuwawchangiaji wa NHIF..je! Kuna mpango gani wa matibabu ? Au ndio tumestaafu hata NHIf