MADUDU YA MWAKYEMBE NA SITTA YAMFIKIA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Rais John Magufuli |
RAIS John Magufuli ndio mtu pekee atakaye awaokoa
Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM , Samwel Sitta na Dk Harrison
Mwakyembe, wote kwa pamoja ambao wanatuhumiwa katika kuitia hasara serikali katika
ununuzi wa Mabehewa mabovu.Mtandao huu unaripoti.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Sitta na Mwakyembe ambao walikuwa mawaziri wa awamu
ya iliyopita chini ya Utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete wanatajwa
kushindwa kuwasimamia wakurugenzi wa shirika la reli kati TRL kwenye ununzi wa
Mabewa ambayo yanatajwa ni mabovu,
Ambapo Mwakyembe naye anatuhumiwa kuhusika au kuzembea
kusimamia watendaji katika ununuzi wa
Mabehewa ya mizigo 274 ambayo yaligharimu serikali bilioni 230 za kitanzania ,
Huku Sitta naye anatajwa kuhusika au nae pia kuzembea kwenye
ununuzi wa mabehewa mapya ya kubebea mafuta kutoka kwenye kampuni ya India
inayojulikana Hindustan Engeering and
indusrial limited ,
Kwa mujibu wa Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban
mwijaka amewaambia wanahabari mabehewa
hayo 50 yalipojaribiwa kwa mara moja tu mabehewa matano yakaanguka njiani jambo
analodai endapo wangeendelea kuyajaribu kwa mara tano basi uwenda mabehewa
mengi zaidi yangeanguka.
Taarifa za kuaminika kutoa ndani ya Serikali
zinasema madudu ya Dkt Mwakyembe na Sitta yamefika Ikulu ya Magufuli ili kuamua
hatma ya vigogo hao wa CCM,
“Ninacho kwambia ila suala la Mabehewa limefika
Ikulu na sahivi kinachosubiliwa ni maamuzi ya Mkubwa tu,maana hakuna jinsi
maana ufisadi huo ni balaa, hapo sio wa mtu mmoja ni wengi wamo humu,wewe unazani mkurugenzi
pekee wa TRL anaweza kuruhusu Pesa zote hizo,:”kimesema Chanzo chetu,
Kuibuka kwa Kashfa hii mpya ya Mabehewa Mabovu
mengine kuna kuja ikiwa ni teyari,Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta
kuunda tume iliyochunguza Mabehewa ya awali na 274,ambapo Kamati hiyo ilikuja
na majibu ambayo Sitta aliwasimamisha kazi vigogo wa TRL,
Vigogo hao ambao ni Mkurugenzi Mtendaji Kipallo
Kisamfu,Mhandisi mkuu wa mitambo Ngosowile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu
Mbaraka Mchopa,
Wengine ni Mkaguzi mkuu wa
ndani wa Kampuni Jasper Kisiraga,pamoja Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinard Soka,
Licha ya Sitta kuwasimamisha wakurugenzi hao
aliahidi kuwawatafikishwa mahakamani ili hatua za kisheria wachukuliwe,
Lakini Jambo la kushangaza ni tayari ni miezi mitano
imepita hakuna hata mkurugenzi yeyote kati ya hao waliyefikishwa mahakamani,
jambo linazidi weka shaka kuhusu sakata hilo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni