MFUMUKO WA BEI JUU,OFISI YA TAKWIMU YASEMA HALI SIO NZURI KABISA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi
wa habari juu ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba ambao umefikia asilimia 6.6
leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Meneja wa Mfumuko wa Bei wa NBS
, Ruth Minja.
MFUMUKO wa bei wa Taifa
kwa Novemba 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia
6.3 ya Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Epharaim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa
mwaka ulioishia Novemba.
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa ya za
vyakula na vinywaji Baridi Novemba mwaka
imeongezeka kwa asilimia 11.2 kutoka asilimia 10.2 tofauti na mwezi
uliopita
Amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa Novemba
2015 kumechangiwa na kuongezeka kwa baadhi ya bidhaa za vyakula
kwa kipindi cha mwezi uliopita zikilinganishwa na bei za Novemba
mwaka jana.
Aliongeza kuwa mwenendo wa bei za baadhi ya
bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka Novemba 2015 ukilinganishwa na bei za
Novemba 214 ni pamoja na mchele kwa asilimia 25.8, Mahindi asilimia
16.4, unga wa mahindi asilimia 12.0 nyama asilimia 8.7, Samaki
asilimia 21.4, Mharagwe asilimia 14.5 Choroko asilimia 15.3 Mihogo
asilimia 10.7 pamoja na viazi vitamu 23.4.
Kwesigabo
amesema kuwa uwezo wa sh.100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.62.31
mwezi Novemba, 2015 kutoka Septemba 2010 ikilinganishwa na Sh.
tofauti na Novemba mwaka jana sh.100 uwezo wake ulikuwa ni
sh.62.82 ilivyokuwa Oktoba 2015.
Mfumuko
wa bei Afrika Mashariki,nchi ya Kenya kwa Novemba
imeongezeka kwa asilimia 7.32, kutoka asilimia 6.72 ya Oktoba mwaka
huu, Uganga imeongezeka hadi asilimia 9.1kutoka asimia 8.8 ya mwezi
uliopita hali hiyo inafanya nchi ya Uganda kuwa ya kwanza kwa
kuongeza mfumuko wa bei.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni