KAMATI KUU YA CCM YAWALINDA MWAKYEMBE NA SITTA,MADUDU YAO TPA NA TRL KUSAFISHIKA,SOMA HAPO KUJUA
DKT Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta ambao
walikuwa mawaziri wandamizi kwenye Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao
kwa sasa wanatuhumiwa kwenye Kashfa za ufisadi, imefichukua kuwa uwezekano wa kupandishwa mahakamani watu hao “
umeyeyuka”.Mtandao umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Sababu iliyotajwa ya kuwaokoa mawaziri hao imetokana
na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,CC kilichoketi jana kimekuja na
mipango mahususi ya kuwaokoa viongozi hao wanajiita na kuitwa ni waadilifu.
Taarifa
za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambazo zimevuja zinasema Kamati ya CC
licha ya kujadili mambo mbali mbali ila jambo la ufisadi ambao uliibuliwa
kwenye Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kashfa ya ununuzi wa mabehewa 250 ya
mizigo pamoja na Mabehewa 50 ya kubebea mafuta ambayo yamebainika kwa sasa ni
mabovu nalo lilizungumziwa.
Chanzo
chetu hicho kilichokuwa ndani ya CC kimedai kuwa viongozi wa mkutano huo walitaka
suala la kuwachukulia hatua mawaziri hao waliokushika nafasi ya wizara ya
uchukuzi,litazamwe kwa umakini kwani linaweza kukiingiza chama hicho tena
kwenye mgogoro.
“Yaani
CC wameona hawa wakina mwakyembe na Sitta wakipandisha Mahakamani kujibu tuhuma
hizo,basi chama chetu kitaingia kwenye mgogoro ambao unaweza hata ukapelekea
idara hata ya Ikulu ya kipindi kile
kufika mahakamani maana ufisadi huu wa Mabehewa ni mkubwa sana na umefanywa na
mtandao mkubwa ndani ya nchi”kimesema Chanzo chetu hicho.
Hata
hivyo Kamati hiyo ya CC licha ya kuwakingia kifua mawaziri hao kunakuja ni
ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi ya Bandari
ambayo Samwel Sitta wakati yupo Uchukuzi aliiunda Bodi ambayo Magufuli ameivunja
kutokana na kuhusika kwenye ufisadi,
Hatua
nyingine kwa bandari hiyo ni Rais Magufuli kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu
wa Bandari Awadh Massawe baada ya kubainika pia ameshindwa kuisimamia Bandari
hiyo kwa kupelekea Ufisadi wa kutisha ikiwemo upotevu wa Kontena zaidi ya 2000.
Sanjaria
Bandarini hapo Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi,Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi
Shaaban Mwinjaka kutokana na kuitia hasara serikali ya bilioni 16 kwenye
sherika la Reli ya Kati TRL.
Taarifa
zilizopatikana wiki iliyopita zilisema Rais Magufuli alikuwa tayari amekabidhiwa
ripoti ya Ufisadi wa Bandarini na TRL ambao unatajwa kuwa kwa namna yoyote
uwezi ukawaacha mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi,
“Hata
ufanyaje ndugu,kwenye ufisadi wa huu wa kutisha lazima Sitta na Mwakyembe “watawabwa
Msalabani tu”,maana wakati makontena hayo yanapoteka kati ya 2014 na 2015
mawaziri hawa walikuwepo uchukuzi hivi hawakuyaona haya au nao kuhusika katika
kubariki wizi huu,harafu ukitoka kwenye Bandari unakuja kwenye TRL hapa ndio
kuna madudu ambayo yanawaacha watupu,wanaojiita wapiganaji wa ufisadi”amesema
Mchambuzi wa Siasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,John Shilima.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni