EU YAIPA TENA MASHARTI TANZANIA,YAITAKA KUMALIZA HARAKA MTIFUANO WA ZANZIBAR,SOMA HAPO KUJUA
Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
(EU EOM) kwa Tanzania unatoa tena wito kwa ukamilishwaji haraka wa mchakato wa
uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za uwazi,
zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika.
Kufuatia Siku ya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, Ujumbe
wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya umebaki nchini kufuatilia chaguzi
zilizoahirishwa Tanzania Bara na mchakato uliyositishwa Visiwani Zanzibar,
baada ya tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) la tarehe 28
Oktoba, lililofuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar.
EU EOM ilikutana na wadau wakuu Visiwani,
vikiwemo vyama vya siasa, Mwana Sheria Mkuu wa Serikali wa zamani na wa sasa,
wadau wa sharia na mahakama, asasi za kiraia na maafisa uchaguzi. Bahati mbaya
EU EOM haikuweza kukutana na Mwenyekiti wa ZEC.
EU EOM inafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea
kati ya CCM na CUF, yanayowashirikisha Marais Wastaafu wa Zanzibar. EU EOM
inarudia tena wito uliyotolewa kwa pamoja na jumbe zingine za uangalizi za
kimataifa tarehe 29 Oktoba, unaoishauri ZEC kuonyesha uwazi kamili kufuatia
uamuzi wake wa kufuta uchaguzi na uongozi wa kisiasa Zanzibar kuweka maslahi ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwanza, kwa lengo la
ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi, kulingana na kanuni za
kidemokrasia za chaguzi pamoja na sheria za Zanzibar.
“EU EOM imekuwepo nchini tangu 11 Septemba
kufuatilia mchakato wa uchaguzi ndani ya Muungano na Zanzibar. Idadi kubwa ya
waangalizi 141 wa EU nchini walirejea Ulaya katikati ya mwezi Novemba, lakini
timu ndogo ya watathmini wa uchaguzi ilibaki nchini kufuatilia ngazi zilizobaki
za mchakato wa uchaguzi,” alisema Muangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Sargentini.
“Japokuwa mchakato wa uchaguzi Zanzibar
haujakamilika, EU EOM itarejea Ulaya kwa muda tarehe 8 Desemba. Umoja wa Ulaya
unaendelea hata hivyo, kuunga mkono kikamilifu mchakato wa uchaguzi Zanzibar na
kwa mchakato mpana zaidi wa kidemokrasia Tanzania. EU EOM iko tayari kurejea na
kuangalia mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea na
mchakato huo yanayolingana na chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa
wakati na za kuaminika yatakapofikiwa,” aliongeza Muangalizi Mkuu.
EU EOM ilitumwa kufuatia mialiko toka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi
Zanzibar. EU EOM inapenda kutoa shukrani zake kwa NEC kwa kuiongezea muda wake
kupita muda uliyopangwa awali, jambo linaloashiria upana wa wigo na mamlaka ya
EU EOM, ambayo yanahusisha zaidi ya uangalizi wa muda mfupi. Ujumbe ulitoa
tamko lake la awali la mchakato wa uchaguzi tarehe 27 Oktoba.
Tarehe 29 Oktoba, EU EOM, pamoja na jumba zingine za
waangalizi za kimataifa za Umoja wa Afrika, SADC na Jumuiya ya Madola, ilitoa
tamko la pamoja kuhus Zanzibar. EU EOM itawasilisha ripoti kamili ya kina,
ikiwemo mapendekezo kwa chaguzi zijazo, ndani ya miezi mitatu ya kukamilika kwa
mchakato wa uchaguzi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni