Zinazobamba

DOKTA MWAKA AUANGANA NA RAIS MAGUFULI KWENYE USAFI SOMA HAPO KUJUA

IMG_9098
pichani ni DKT Mwaka picha na Maktaba
TABIBU bigwa wa Mgonjwa ya Uzazi nchini,DKT Mwaka leo ameungana na Rais John Magufuli kutekeleza kauli mbio ya kufanya usafi katika kusherekea siku ya Uhuru.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Tabibu huyo anayesifika Nchini alitekeleza kaulimbiu hiyo na Wakazi wa Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa kusafisha Maeneo yote yanayozunguka Hospitari ya Amana,Soko la Karume,soko la Boma pamoja na Barabara zote zilizopo kata ya Ilala,
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa niaba ya Dokta Mwaka,Mke wa Dokta huyo Quen Mwaka amesema wameipokea agizo la Rais la kufanya usafi kwa moyo mmoja ili kuweza kupambana na Ugonjwa wa kipindupindu.
“Tumejumuika wakazi wote wa Ilala kufanya usafi katika kuungana na Rais Magufuli,na tunashukuru mungu wakazi wa Ilala wametuunga mkono na hili ni jambo jema ambalo litatusaidia kuondokana na ugonjwa huu hatari wa kipindupindu”amesema Mama Mwaka.

Kwa upande wake wa Kazi wa kata ya ilala waliojiunga na Dkt Mwaka kufanya usafi maoneo hayo,wammpongeza Dkt Mwaka kwa hatua aliyochukua ya kuwaunganisha ili waweze kutekeleza Agizo la Rais Magufuli lilowataka kufanya usafi.

Hakuna maoni