Zinazobamba

MBUNGE SAED KUBENEA AKAMATWA NA POLISI,NI BAADA YA MTIFUANO NA DC MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA


MBUNGE  wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea amekamatwa na polisi baada ya kutolewa amri ya kukamatwa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Paul Mkonda.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

    Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana  kwenye kiwanda cha kimoja kilichopo meneo ya Ubungo Jijini Dar es Salaam,ambapo inaelezwa kuwa wafanyakazi wa Kiwanda hicho ambao walimuomba Mbunge wao ambaye ni Kubenea afike kwenye kiwanda hicho,ili wamweleza matatizo yao wanayokumbana nao ili Mbunge wao aweze kuwasaidia.

      Ambapo Kubenea alipofika kiwandani hapo kutii amri ya wananchi wake.mara ya baada ya kufika  alimkuta DC Makonda ambaye naye alikuwepo Kiwandani hapo akiongea na wafanyakazi hao,ambapo mara baada ya Makonda kumaliza kuongea na wafanyakazi hao ndipo kelele zilisikika kutoka kwa wafanyakazi hao, wakitaka mbunge wao ambaye ni Kubenea ili ongee na wao wapate nafasi ya kutoa madukuduku yao

“Tunamtaka mbunge wetu Kubenea aongee maana ndio tumemchagua kwa kura zetu tunamtaka Kubenea”kelele za Wafanyakazi hao zilisikika.

      Mara baada ya kelele hizo ndipo DC Makonda alipinga Kubenea kuongea bila hata kutaja sababu ya kumzuia Mbunge huyo,Jambo ambalo Kubenea alilipinga huku akisema "mimi nimeitwa na wapiga kura wangu ili waweze kunieeleza matatizo yao" na ,akahoji kwa kusema "inakuwaje unikatalie?,"

      Licha ya Kubenea kujitetea huku,,bado DC Makonda akashikilia msimamo wake wa Mbunge huyo kutoongea na wapiga kura wake,ambapo jambo hilo alizidi kulipanga tena  Kubenea ,ndio sababu iliomfanya DC Makonda kutoa matusi machafu kwa kubenea na kuamulu Polisi wa kituo cha Magomeni kumkamata kubenea,
     WakatiMakonda akitoa amri hiyo Kubenea aligoma kukamatwa na Polisi huku akisema haoni kosa lake yeye kukamatwa ndipo Polisi wakatumia nguvu kumkamata na kufanikiwa kuondoka naye mpaka kituoni Magomeni.

Mpaka taarifa hii inaripotiwa Mbunge Kubenea Bado aliendelea kusota Kituoni hapo.

            WANAHABARI WANYANYASWA.
Katika hali ya kushangaza waandishi wa habari waliokuwa eneo hilo nao walikumbwa na kadhia ya kunyanyaswa baada ya DC Mkonda kuamulu kamera za waandishi wa habari wa Star TV na Sibuka Tv pamoja na Mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima ambao walikuwa wakirekodi tukio nzima kunyang’anywa kamera zao.


Maoni 2

Unknown alisema ...
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
UJUZI NA MAARIFA (skills & knowledge) alisema ...

huyo jamaa ni dictator, anapenda kutumia vbaya madaraka, huyu hafanyi kazi bali ni ubabe na unyanyasaji, ALIWAHI KUMPIGA WARIOBA NDIO AKAPEWA UKUU WA WILAYA. naskia yupo kwenye system, boya tu