MBUNGE SAED KUBENEA AKAMATWA NA POLISI,NI BAADA YA MTIFUANO NA DC MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA
MBUNGE wa
Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea amekamatwa na polisi baada ya kutolewa amri ya
kukamatwa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Paul Mkonda.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Tukio hilo
limetokea leo majira ya mchana kwenye
kiwanda cha kimoja kilichopo meneo ya Ubungo Jijini Dar es Salaam,ambapo
inaelezwa kuwa wafanyakazi wa Kiwanda hicho ambao walimuomba Mbunge wao ambaye
ni Kubenea afike kwenye kiwanda hicho,ili wamweleza matatizo yao wanayokumbana
nao ili Mbunge wao aweze kuwasaidia.
Ambapo
Kubenea alipofika kiwandani hapo kutii amri ya wananchi wake.mara ya baada ya kufika alimkuta DC Makonda
ambaye naye alikuwepo Kiwandani hapo akiongea na wafanyakazi hao,ambapo mara
baada ya Makonda kumaliza kuongea na wafanyakazi hao ndipo kelele zilisikika kutoka kwa
wafanyakazi hao, wakitaka mbunge wao ambaye ni Kubenea ili ongee na wao wapate
nafasi ya kutoa madukuduku yao
“Tunamtaka mbunge wetu Kubenea aongee maana ndio
tumemchagua kwa kura zetu tunamtaka Kubenea”kelele za Wafanyakazi hao
zilisikika.
Mara
baada ya kelele hizo ndipo DC Makonda alipinga Kubenea kuongea bila hata kutaja
sababu ya kumzuia Mbunge huyo,Jambo ambalo Kubenea alilipinga huku akisema "mimi nimeitwa na wapiga kura wangu ili waweze kunieeleza matatizo yao" na ,akahoji kwa
kusema "inakuwaje unikatalie?,"
Licha ya
Kubenea kujitetea huku,,bado DC Makonda akashikilia msimamo wake wa Mbunge huyo
kutoongea na wapiga kura wake,ambapo jambo hilo alizidi kulipanga tena Kubenea ,ndio sababu iliomfanya DC Makonda kutoa
matusi machafu kwa kubenea na kuamulu Polisi wa kituo cha Magomeni kumkamata
kubenea,
WakatiMakonda
akitoa amri hiyo Kubenea aligoma kukamatwa na Polisi huku akisema haoni kosa
lake yeye kukamatwa ndipo Polisi wakatumia nguvu kumkamata na kufanikiwa
kuondoka naye mpaka kituoni Magomeni.
Mpaka taarifa hii inaripotiwa Mbunge Kubenea Bado aliendelea kusota Kituoni hapo.
WANAHABARI
WANYANYASWA.
Katika hali ya kushangaza waandishi wa habari
waliokuwa eneo hilo nao walikumbwa na kadhia ya kunyanyaswa baada ya DC Mkonda
kuamulu kamera za waandishi wa habari wa Star TV na Sibuka Tv pamoja na Mpiga
picha wa Gazeti la Tanzania Daima ambao walikuwa wakirekodi tukio nzima kunyang’anywa
kamera zao.
Maoni 2
huyo jamaa ni dictator, anapenda kutumia vbaya madaraka, huyu hafanyi kazi bali ni ubabe na unyanyasaji, ALIWAHI KUMPIGA WARIOBA NDIO AKAPEWA UKUU WA WILAYA. naskia yupo kwenye system, boya tu
Chapisha Maoni