MAWAZIRI WA MAGAFULI WAWA MBOGO,MWALIMU NA KIBWANGALLAH WATEMA CHECHE,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangallah |
WAZIRI wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa
mikoa, wilaya na kata kuhakikisha wanakuwa na kikosi kazi cha kupambana na
kipindupindu na kutoa ripoti ya utekelezaji kwa ngazi za juu kila siku. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Mwalimu ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wanahabari
katika makao makuu ya wizara yake kuhusu namna ya kuzuia usambaaji wa mlipuko
wa kipindupindu.
Amesema kuwa pamoja na kuwa na kikosi hicho, viongozi na
watendaji wa mikoa na halmashauri wasimamie majukumu yao ya kukagua na
kusimamia usafi katika kila kaya na kila siku ili kuboresha hali ya usafi na
kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka.
Mwalimu amesema shule zote pamoja na vyuo vinavyoendelea kutoa
mafunzo na taasisi mbalimbali zizingatie kanuni za afya ili kuzuia ugonjwa
usiingie katika maeneo yao.
Tangu ugonjwa huu uanze jumla ya watu 11,257 walipata ugonjwa
huu na kati yao jumla ya watu 177 wameshafariki ambao ni sawa na 1.5% ya
waliougua.
Aidha Mwalimu alitaja mkoa ambao umekuwa na wagonjwa wengi tangu
mlipuko uanze ni Dar es Salaam 4628 ambayo ni 41% ya wagonjwa wote, ikifuatiwa
na Tanga 1443 ambayo ni 13%, Singida 955 ambayo ni 8%, Mwanza 841 ambayo ni 7%.
Katika mazungumzo hayo pia Mwalimu amepiga marufuku uuzaji wa
matunda yaliyomenywa na chakula katika maeneo ya wazi kutokana na kuibuka kwa
kasi ya ugonjwa huo.
Ameagiza pia maafisa afya kuhakikisha wauzaji wote wa vyakula
wanazingatia kanuni za usafi ikiwa ni pamoja na kuosha vyombo kwa maji salama
na yamoto na sabuni.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni