MAGUFULI AANZA KUWAFUKUZA KAZI MCHWA WA KIKWETE,RUNGU LAMWANGUKIA HOSEAH,SOMA HAPO KUJUA
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hoseah |
RAIA wa
Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Dk. Edward Hoseah kutokana
kutoridhishwa na utendaji wa taasisi chini ya uongozi wake. Anaandika Erasto Masalu … (endelea).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu, imemnukuu Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuwa kufuatiwa na kutenguliwa kwa uteuzi
huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo,
Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Balozi Sefue amebainisha kuwa Rais Magufuli amechukua hatua hiyo
baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wa Takukuru chini ya Dk. Hoseah hauwezi
kuendena na kasi anayoitaka.
“Eneo mojawapo la upotevu mkubwa wa mapato ni Bandari ya Dar es
Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini Rais Magufuli (John)
amesikitishwa na Takukuru kushindwa kuchukua hatua yoyote,” amesisitiza
Balozi Sefue.
Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema Rais Magufuli
ameagiza kusimamishwa kazi mara moja maafisa wanne wa Takukuru ambao walisafiri
nje ya nchi pamoja na kuwepo agizo la rais kuzuia safari za nje ya nchi.
Watumishi hao waliosimamishwa kazi ni Mary Mosha, Ekwabi
Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya
kunyimwa kibali cha kusafiri kutoka kwa Rais au Katibu Mkuu Kiongozi.
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii
agizo la Rais Magufuli na kuwaonya atakayeenda kinyume na agizo hilo
atachukuliwa sheria kali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni