BENKI YA NMB YAZINDUA MFUMO WA KISASA WA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MIKOPO, WATEJA SASA KUPATA MIKOPO NDANI YA SIKU 4.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa
Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na
Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo (
CRB's) na kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kutoka NMB
kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 kutokana na taarifa zao za mikopo kuendelea kuwepo kwenye mfumo wa Benki hiyo.
Afisa Mkuu
Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya
NMB inavyoongoza katika utoaji wa mikopo
kwa makundi mbalimbali.
Kaimu
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela( kulia) akitoa
ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo
kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa
kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker .
(Na.Aron
Msigwa - Dar
es salaam).
Benki
ya NMB imezindua mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za wateja utakaotumika kwenye
kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB's) kwa lengo la kuwawezesha wateja
wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na
ilivyokuwa mwanzo kutokana na taarifa
zao zao za mikopo kuwepo kwenye mfumo wa Benki hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NMB Plc Ineke Bussemaker amesema kuwa utaiwezesha Benki hiyo kuwahudumia wateja
wake katika matawi zaidi ya 170 yaliyoko nchi nzima kwa haraka zaidi tofauti na
kuiwezesha Benki hiyo kuwasiliana na benki nyingine kwa njia ya mtandao.
"
NMB tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya utoaji wa huduma ili kuwapatia wateja
wetu huduma bora, kulingana na utendaji wa mfumo huu mteja wetu sasa atapata
mkopo wake ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma ambapo
ilichukua takribani wiki mbili mteja kupata mkopo wake"
Amesema
kuwa Benki hiyo husshughulikia maombi ya mikopo zaidi ya 700 kwa siku na
kuongeza kuwa kupitia mfumo huo wa kisasa taarifa za huduma ya utoaji wa mikopo
ndani ya NMB, mishahara ya wafanyakazi inayopitia Benki hiyo, waombaji wadogo
na Wakubwa wa mikopo hiyo ikiwemo wafanyabiashara na makampuni zitadhibitiwa kutokana na uwepo
wa mifumo huo wenye uwezo wa kuchambua na kuweka kumbukumbu za wateja wanaoomba
na kurejesha mikopo kwa haraka.
Aidha
amesema kupitia matumizi ya Mfumo huo (
Simbuka) Benki ya NMB itaweza
kufuatiliaji taarifa za wateja kwa ukaribu zaidi.
Kwa
Upande wake Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols
amesema kuwa Benki ya NMB inaongoza
katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali nchini kwa mikopo
inayofikia shilingi Trilioni 2.2 kwa mwaka ambapo asilimia 25 ni mikopo midogo
na asilimia 25 ni mikopo kwa wateja
wakubwa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu madai ya kiwango cha riba kinachotolewa na Benki za Tanzania
kuwa kikubwa ameeleza kuwa kiwango hicho kinachangiwa na hali ukuaji wa uchumi wa eneo husika pamoja na gharama za kupata amana za mikopo na kutoa
wito kwa mabenki kote nchini kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha utoaji wa
huduma za kibenki nchini.
Kaimu
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela akitoa
ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo huo amesema umejengwa kwa ushirikiano na
wataalam kutoka Nethaland,unawezesha ushirikiano wa taarifa za kibenki kutoka
benki moja kwenda nyingine na sasa wateja watapata mikopo yao ndani ya siku 4 kutokana na taarifa za mifumo kuwasiliana.
Aidha,
amesema mabadiliko hayo yameanzishwa na Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) yamechukuliwa kwa umakini na Benki
hiyo kutokana na idadi kubwa ya mikopo na wateja inaowahudumia.
Aidha,
amesema kuwa mtandao huo utasaidia Benki
ya NMB kufuatilia na kubainisha mwenendo wa wateja wanaolipa vizuri na vibaya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni