MAWAKA WA FORODHA WADAI WIZI WA KONTENA 2431 UNAWAHUSU WATENDAJI WA BANDARI, ATAKA SERIKALI KUWACHUNGUZA.
Chama cha mawakala wa forodha Tanzania (TAFFA) kimeelezea kusikitishwa kwake na hatua za kukamatwa kwa wanachama wake wapatao 73 kwa kigezo cha kukwepa kulipa kodi, wakati ukweli ni kwamba watu hao wamelipa kodi na vielelezo vyote wanavyo vinavyoonyesha kutekeleza ulipaji huo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Rais wa chama cha mawakala wa forodha Bw. Stephen Ngatunga amesema wanashangwazwa na hatua zinazoendelea za kukamata makampuni zaidi ya 73 ambayo yanadaiwa kukwepa kodi wakati tayari wamelipa kodi hiyo.
Alisema kumekuwa na lawama nyingi zinazoelekezwa kwa wanachama wa TAFFA wakidaiwa kukwepa kulipa kodi suala ambalo rais Katunga amelikanusha na kusema wizi wa bandari unawahusisha moja kwa moja wafanyakazi wa Bandari(TPA) na wafanyakazi wa benki zilizoruhusiwa kukusanya tozo hizo.
Aidha Katunga ameiomba serikali kushirikiana na chama hicho ili kuwezesha kubainika kwa mianya ya wizi iliyokuwa ikifanywa na watendaji wa bandari na benki, kwani hivi sasa kumekuwa na jitihada za kuficha ukweli na kuwakomoa wanachama wa TAFFA.
Katika hatua nyingine, Katunga amemtaka Mkuu wa Bandari kuacha kutoa maagizo ya kukamatwa kwa wanachama wake na badala yake achukue risiti na nyaraka na kuanza kuzifanyia kazi ikiwamo kuhakiki kama fedha ni kweli zimelipwa katika benki husika.
Amesema alitaraji Mkurugenzi wa TPA angefanya kazi kwa kushirikiana na mawakala wa forodha ili kubaini ukweli lakini kinyume chake amekuwa akiwakamata na kuzuia kufanya kwa biashara kwa kampuni hizo.
Wamelipa na risiti wanazo, ni kitendo cha kuchukua risiti zao na kwenda kuzifanyia uhakiki, sasa kuwakama haitasaidia. Alisema Katunga.
Ngatunga akifafanua utata wa mkurugenzi wa Bandari kuanza kutoa agizo la kukamatwa kwa wanachama wa TAFFA huku waliosababisha upotevu wa makontena wakibaki Salama. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni