HUJUMA ZA UMEYA KWA UKAWA,CHADEMA WAIBUKA WAMUANGUKIA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Diwani kata ya Mwanzange, Rashid Jumbe (CUF) ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya Umeya wa jiji la Tanga akipiga kura |
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimemtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu yaliyopo ofisini kwake kutokana na
watumishi wa serikali kutumika kuvuruga chaguzi za mameya kwenye miji
mbalimbali nchini. Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar
es Salaam na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene alipozungumza na
waandishi wa habari na kwamba, katika maeneo mengi ya chaguzi ambayo vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa na nafasi ya kutwaa umeya
wa Halmashauri au Jiji, CCM hufanya vurugu.
Amesema
kuwa, ofisi ya rais yenye sifa ya ‘kutumbua majipu’, inapaswa kutumbua majipu
yanayohitajika kutumbuliwa licha ya kuwa yeye mwenyewe anaweza kuhusika kwenye
zoezi hilo.
“Vurugu
hizo zinaratibiwa kwenye ofisi ya rais kama sio rais mwenyewe kuhusika. Cha
kushangaza halichukulii hatua suala hilo ambapo tunapata mashaka ya kuhusika
kwake kwenye vurugu hizo kutokana na kuwa mambo hayo yanaendelea kwenye ofisi
yake,” amesema Makene.
Amesema
kuwa, Jiji la Tanga tangu jana limekuwa likizuungukwa na polisi wa doria wenye
risasi na mabomu hali ambayo inawatia hofu wakazi wa jiji hilo.
Amesema
kuwa, Jeshi la Polisi limekuwa na tabia ya kukilinda Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambao wamejijengea tabia ya kutumia jeshi hilo kulinda maslahi yao binafsi.
Wakati
huo huo Makene amesema kuwa, Chadema inalaani uvunjwaji wa matawi ya chama chao
na ushushwaji wa bendera unaoendele kwenye Jimbo la Ruangwa kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni amri ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kassimu ambaye ni mbunge wa
jimbo hilo.
Majaliwa
amewekwa jimboni mwake katika kile kilichoelezwa kuwa yupo kwenye mapunziko ya
siku 10 jimboni humo.
Makene
amesema kuwa, vitendo hivyo ni viashiria vya ukandamizaji wa demokrasia na haki
za wananchi ambapo waziri mkuu ameamuru watu kuchochea fujo kwa kuwataka wasiwe
wafuasi wa chama kingene cha siasa ambapo ni kinyume na cha haki.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Maoni 1
haki itendeka
Chapisha Maoni