MAREKANI YAMWOGOPESHA MAGUFULI,AAMUA KUMUITA MAALIM SEIF IKULU,SOMA HAPO KUJUA
MAALIM Seif Shariff Hamad ambaye anapigania haki
yake ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar baada ya uchaguzi huo
kufutwa kihujuma, amekutana na Rais John Magufuli leo Ikulu jijini Dar es
Salaam. Anaandika Jabir Idrissa …
(endelea).
Ni mkutano wa faragha
uliomhusisha pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan ambaye Dk. Magufuli aliahidi kushirikiana naye pamoja na Dk. Ali
Mohamed Shein kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar.
Maalim
Seif amekuwa akishiriki vikao vya faragha na viongozi wastaafu wa Zanzibar,
pamoja na Dk. Shein ambaye ameendelea kubaki madarakani licha ya madai kuwa
urais wake ulikoma kisheria tangu Novemba 2.
Vikao
ambavyo Maalim Seif amekuwa akishiriki pamoja na Dk. Shein, ndani ya Ikulu ya
Zanzibar, vimehusisha pia marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour
Juma na Amani Abeid Karume, ambaye alishirikiana naye kujenga siasa za
maridhiano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hakuna
taarifa iliyotolewa na upande wowote baada ya kikao cha Maalim Seif na Rais
Magufuli, lakini mazingira yanaonesha kuwa ni hatua za dhati za kiongozi huyo
mpya za kusimamia utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar.
Rais
Magufuli aliahidi wakati wa kuzindua Bunge la 11 mjini Dodoma kuwa kuna tatizo
linapaswa kushughulikiwa Zanzibar na mbali na makamu wake wa rais, Samia,
atashirikiana na Dk. Shein.
Mkutano
wake na Maalim Seif unafanyika katika wakati ambao wananchi wamekuwa wakisubiri
kwa shauku kubwa kujua hatima ya mgogoro uliotokana na hatua ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kuufuta uchaguzi wa Zanzibar
uliofanyika Oktobva 25.
Taarifa
yake hiyo imepingwa kwa nyanja mbalimbali, ikianzia na wanasheria wa ndani ya
Tanzania, serikali za kimataifa na wananchi, wakisema hakuna mamlaka yoyote ya
kisheria yanayompa haki ya kufanya hivyo.
Chama
cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kimesema Jecha hana mamlaka hayo kwa sheria
yoyote wala katiba ya Zanzibar, na anapaswa kufuta tamko lake ili Tume
ikamilishe kazi ya kuhakiki kura zilizobakia na kutangaza matokeo yake pamoja
na mshindi wa nafasi ya urais.
Alipotoa
tangazo la kufuta uchaguzi Oktoba 28, Jecha alikuwa ameshatangaza matokeo ya
urais ya majimbo 33, ambayo wawakilishi wake walishapatiwa vyeti vya ushindi
pamoja na majimbo mengine yote yaliyobaki. Zanzibar ina majimbo 54 ya uchaguzi.
Maalim
Seif na chama chake Chama cha Wananchi (CUF) wanasema Jecha alishinikizwa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuufuta uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa
kilishapoteza madaraka kwa kushindwa uchaguzi.
CCM
imekuwa ikishikilia kuwa Tume itangaze tarehe ya kufanyika uchaguzi mpya,
shinikizo ambalo watendaji wa Tume wanasema hawawezi kulifanyia kazi kwa kuwa
hawajapatiwa fedha za maandalizi ya uchaguzi huo.
habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni