WAZIRI WA MAGUFULI AMUUMBUA KIKWETE,NI KUHUSU MAJINA YA VIGOGO WAUZA MADAWA YA KULEVYA NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada
ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini.
|
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi, Charles Kitwanga
ni kama amemruka Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuhusu uwepo wa orodha ya majina ya vigogo wanaouza madawa ya kulevya nchini, baada ya kusema hakuna orodha ya majina
hayo,
Hata hivyo pia Waziri Kitwanga amewatangazia kihama, watu wote wanajihusisha na uuzaji wa madawa ya
kulevya nchini kwa kusema hata muogopa mtu yeyote na iwe mkubwa wala mdogo wote
atawachukulia hatua.
Akizungumza
na waaandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika mazungumzo na viongozi wakuu wa jeshi la polisi nchini,ambapo Waziri Kitwanga amesema kwa
sasa hakuna orodha yeyote ya majina ya vigogo wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya
kulevya, kwa kudai kuwa kama orodha hiyo ingekuwepo basi angeshawachukulia hatua za
kisheria.
“Hakuna
orodha ya wauza madawa ya kulevya hapa au hao wanaoitwa vigogo,maana kama
wangekuwepo ningewachukulia hatua, maana simwogopi mtu kabisa awe mkubwa au
mdogo kama unajihusisha na biashara hii lazima tukuchukulia hatua”amesema Waziri
Kitwanga.
Waziri
Kitwanga ameongeza kuwa kwa sasa wizara yake pamoja na kushirikiana na kitengo
cha kupambana na biashara ya madawa ya kulevya nchini wametaka watu wote
wanaofanya biashara hizo kuachana mara moja.
“Nawataka
kabisa watu wote wanaojihusisha na
biashara ya kuuza madawa ya kulevya waache kabisa na wafanya kazi nyengine
maana tumejipanga kupambana nao kufa na kupona na kuhakikisha tunamaliza kabisa
mtandao wote nchini”ameongeza kusema.
Kuibuka
huku kwa Waziri Kitwanga kunakuja ikiwa na miaka minane kupita wakati wa kipindi cha
utawala wa awamu ya nne ambapo Rais Kikwete aliliambia taifa kuwa anamajina ya
vigogo ya wauza madawa ya kulevya nchini na kujiipiza kuwa atawachulia hatua
kali za kisheria.
Jambo
ambalo mpaka Kikwete anaondoka madarakani hakuna hata kigogo mmoja
aliyemchukulia hatua au kumfikisha mahakamani zaidi tu ya wauzaji wadogowadogo
maarufu kama vidagaa tu ndio
wakifikishwa mahakamani huku vigogo wakitesa,
Kauli ya
waziri Kitwanga inatafsiriwa na wachambuzi wa mambo ni kama inamuumbua Rais
mstaafu Kikwete kwa kuonesha alikuwa hana majina hayo sana sana alikuwa anataka
sifa au huruma kwa wananchi.
IGP MANGU
ANENA.
Katika hatua nyengine Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini,Ernest Mangu ametangaza kumsaka mtu aliyesambaza ujumbe kwenye mitandao
ya kijamii akisema jeshi la polisi limewasimamisha wafanyakazi wake 300 kwa
madai ya kugushi vyeti.
“Taarifa ambazo hizo ni za uongo,na kwa sahivi
tunamtafuta mtu alisambaza ujumbe huo ili tumchukulie hatua za kisheria”amesema
IGP,Mangu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni