Zinazobamba

YAMETIMIA SASA WASANII KUNUFAIKA NA NYIMBO ZAO KUCHEZWA REDIONI,SOMA HAPO KUJUA

Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akijibu moja 
ya maswali katika semina hiyo. Mutahaba aliwahamasisha wanamuziki 
kujisajili CMEA kwa lengo la kupata haki  kutokana na kazi zao
Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya 
CMEA.
   Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.
    Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo  itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine  katika taasisi mbalimbali.
       Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili  kuhakikisha kila mwanamuziki  anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati  ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya  redio.
   Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo  vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.


“Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za  mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa  wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine 
pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse  alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha  kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni  na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa 
malengo maalum.
  “Pia  tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya  uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo  vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya 
urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

Alisema kuwa  wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki
zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika 
redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili, 
kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,” 
alisisitiza.

Hakuna maoni