Zinazobamba

ZITTO KABWE AMPOPOA MAGUFULI NA ZIARA ZAKE,AENDELEA KUMTAITISHA KUHUSU MGOGORO WA ZANZIBAR,SOMA HAPO

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo


NA KAROLI VINSENT
IKIWA ni siku tano tu tangu Rais John Magufuli kuanza kufanya kazi yake ya Urais ndani ya Ikulu,Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ni kama ameanza kumbana Magufuli kwa kusema ziara zake za kushtukiza alizozianza kwenye ofisi mbali mbali za umma hizitakuwa na  tija kwa Taifa kama endapo ataendelea kulifumbia macho sakata la Zanzibar.
       Zitto ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema ni jambo la kushangaza kuona Rais Magufuli anapita kwenye wizara na mahospitali huku hakishindwa kutatua mgogoro ambao unaitikisa dunia kwa sasa ambao upo visiwani Zanzibar.
      “Rais Magufuli angetakiwa kabisa kitu cha kwanza cha kufanya baada ya kuingia ofisini ni kutatua mgogoro wa Zanzibar maana Zanzibar ni miongoni mwa maeneo yanaiunganisha Tanzania,ambacho anafanya leo kupita kwenye ofisi za umma  itakuwa haina maana bila kutatua mgogoro huu”
      Amesema kuwa Rais Magufuli wakati anaapishwa ameapa kwa kusema atailinda na kutetea Katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania lakini  ameshangazwa ni  kitendo cha  Magufuli kumfumbia macho mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,Jecha salum Jecha kuvunja katiba ya uchaguzi pamoja na Zanzibar Kwa kufuta uchaguzi  ambapo kunakwenda kinyume na katiba ya nchi
        “Leo tunashangaa kiongozi huyo Magufuli kuwa kimya kwa kumwacha Jecha anavunja katiba ya nchi ambayo hakuna hata kipengele kinachompa mamlaka ya kufuta uchaguzi  wa Zanzibar,bila hata ya kushauriana na wenzake huku viongozi wanamtazama ni kitu ambacho hakieleweki”
        Zitto ambaye pia ni Mbunge mteule kupitia Jimbo la Kigoma Mjini amedai Katiba ya Zanzibar imeshaeleza ukomo wa Rais Sheni ni kwamba unafikia tarehe 2 ya mwezi huo ,lakini kitendo cha Dk Sheni kujibatiza kuwa Rais mpaka leo, amesema ni  jambo linalovunja katiba na amemtaka  Rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kumshitaki Dk sheni kama “Mhaini”
     Mwanasiasa huyo kijana licha ya kumtaka Magufuli kuingilia kati mgogoro huo pia amemshahuri  Magufuli kuwa  kama atashindwa kutatua mgogoro huo basi atangaze hali ya hatari Visiwani Zanzibar maana Katiba inampa Mamlaka hayo.
     “Kama suala hili limekuwa gumu kwake Magufuli,basi atangaze hali ya hatari tujue,maana ikitangazwahivi ili ipite mda maalum ili Katiba ya Zanzibar itungwe tena na uchaguzi ufanyike tena kuriko kuacha uvunjwavi huu wa Katiba ya wazi”
     Kuibuka kwa mwanasiasa huyo kijana nchini katika kuendelea kupambana na mgogoro wa Zanzibar kunakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya kiongozi wa Umoja wa Mataifa nchini,UN kumtaka mwenyekiti wa ZEC kutangaza matokeo ya uchaguz huo na sio kuyafuta.

   Wakati mgogoro huo unazidi kuitia aibu Tanzania kwenye medani za kimataifa pia ni teyari nchi Wahisani wakiongozwa na Marekani wamatishia kusitisha kiasi cha Dola milioni 900  kwa serikali ya Tanzania endapo itaendelea na uonevu wa Demokrasia visiwani Zanzibar.

No comments