MARAFIKI WA KIKWETE WAANZA KUONDOKA MDOGOMDOGO IKULU,SALVA RWEYEMAME NAYE AKUSANYA VIRAGO,SOMA HAPO KUJUA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu amemaliza mkataba wake na kuondoka huku akiwashukuru watendaji kwa muda wote aliokuwa nao wakimsaidia Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete.
Kuondoka kwake kunampa fursa Rais wa Awamu ya Tano,
Dk John Magufuli kuunda safu mpya ya Kurugenzi ya Mawasiliano. Salva
aliteuliwa, kwa mara ya kwanza, na Rais Kikwete kushika wadhifa huo Septemba
17, 2007 na alimaliza mkataba wake Septemba 11, 2015 lakini aliongezewa hadi
Novemba 10.
Baada ya Dk Magufuli kuapishwa Novemba 5, Rais
Kikwete aliondoka siku iliyofuata kurudi nyumbani kwao Msoga, Chalinze, na kwa
kuwa Salva amemaliza pia muda wa nyongeza ameondoka na kurudia majukumu yake ya
awali.
Kabla ya kuteuliwa kusimamia Kurugenzi ya
Mawasiliano Ikulu Salva alikuwa mmoja wa wamiliki na Mhariri Mtendaji wa
kampuni ya Habari Corporation (sasa New Habari Corporation). Mwaka huo,
aliteuliwa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Peter Kallaghe aliyeteuliwa kuwa
Balozi wa Tanzania nchini Canada.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki
iliyopita Salva aliweka wazi kuwa ataondoka katika ofisi hiyo Jumatatu ya wiki
hii (jana) na kumkaimisha msaidizi wake, Mwandishi wa Rais Msaidizi, Premi
Kibanga kuendelea na majukumu yatakayojitokeza.
“Nimetumika Ikulu kwa zaidi ya miaka minane na kwa
kipindi hicho chote nimesaini mikataba kadhaa ya kuendelea na kazi. Wakati
umefika wa mimi kuondoka. Nawashukuru viongozi wa Ikulu pamoja na Rais Kikwete
aliyeniamini kuwa msaidizi wake. Nampongeza Dk Magufuli pia kwa kuchaguliwa
kwake kuendelea kuwatumikia Watanzania,” alisema Salva ambaye pia aliwahi kuwa
mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya umma ya S & G.
“Mkataba wangu wa mwisho wa kazi uliisha Septemba 11,
2015 kabla sijaongezewa mwingine unaokamilika Novemba 10 na siku hiyo
nitaikabidhi ofisi kwa Premi Kibanga. Nimemaliza kuweka mambo yote sawa tangu
Jumapili. Ninaondoka nikiwa mwenye furaha, nilishirikiana vyema na Makatibu
Wakuu; Philemon Luhanjo na Balozi Ombeni Sefue,” alisema.
Aidha, amewashukuru waandishi wa habari kwa
ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichohudumu kwenye kurugenzi hiyo mpaka
wakati huu anapoondoka
No comments
Post a Comment