ZITTO KABWE AIBUKA NA KUJITOSA MGOGORO WA ZANZIBAR,NAYE AUNGANA NA UKAWA SASA,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WAKATI dunia ikiwa bado inashangazwa na uvunjavi wa
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 baada
ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kwa kufuta uchaguzi mkuu
uliofanyika Octoba 25 mwaka huu visiwani humo,
Ambao
Uchaguzi huo unatajwa kuwa Mgombea kupitia Chama cha Wananchi CUF ambaye
anaungwa mkono na Vyama vya UKAWA,Maalim Sef sharrif hamad kuibuka ushindi
kwenye nafasi ya Urais,
Naye pia
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe ameingilia kati suala hilo
na kumtaka mwenyekiti wa ZEC bwana Jecha kutangaza matokeo yaliyobakia na Rais
wa visiwani humo aapishwe ili kazi iendelee.
Zitto
ambaye ni Mbunge wa kigoma Mjini ameyasema hayo kupitia kupitia Akaunt zake za
mitandao ya kijamii,ambapo amedai inasikitisha kuona katiba ya Zanzibar
inavunjwa hadharani huku hakuna mtu yeyote anayekemea suala hilo.
“Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa,matoke
yatangazwe na mshindi apatikane,hatuwezi kutazama tu katiba
inakanyagwa,Vinginevyo Maalim Sef atafute Jaji amwapishe”
Ameongekwa kuwa “na aunde serikali,mara moja na
kuanza kuwatumikia wanzanibar,serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na katiba”
Kuibuka
huko kwa Mwanasiasa huyo machachali nchini,kunakuja ikiwa ni siku moja kupita
baada ya Wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochaguliwa kwenye uchaguzi huo
uliofutwa kuibuka na kumlaani mwenyekiti wa ZEC kwa kusema amevunja katiba ya
Zanzibar,
Mbali
na wajumbe hao wawakilishi kulaani “ubakaji” wa Demokrasia nchini pia taarifa
zinasema teyari nchi wahisani kuongozwa na marekani wamesitisha msaada wa dola
milioni 900 kwa serikali ya Tanzania mpaka
pale mgogoro huo utakapotafutiwa ufumbuzi.
Licha ya
nchi hizo wahisani ni Teyari jumuiya ya waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa
pamoja na wandani wamelaani kitendo cha mwenyekiti wa ZEC kufuta uchaguzi huo
wakidai amekurupuka na hana mamlaka ya kikatiba kufanya hivyo.
Waangalizi
hao wamesema madai anayosema Jecha kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro hayana
msingi kwani wao walishuhudia uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru na haki.
No comments
Post a Comment