WAKAZI WA DODOMA NAO WAISOMA NAMBA SASA,SHIDA YA MAJI YAZIDI WAMALIZA,SOMA HAPO KUJUA

WANANCHI wa mji
wa Dodoma wameonja joto ya jiwe kwa kukosa maji kwa siku mbili mfululizo huku
wakihofia tatizo hilo linaweza kuwasababishia kukumbwa na ugonjwa wa
kipindupindu ambao kwa sasa ni tishio kwa kila kona ya nchi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
(endelea).
Hali
hiyo ya kukosemana kwa maji katika mji wa Dodoma inatokana na kuwepo kwa
tangazo la Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira, kueleza kuwa kutokana na
kuwepo kwa tatizo la umeme kunasababisha kutopatikana kwa maji katika maeneo
mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Mkazi mmoja wa
Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Yahana amesema kitendo cha
kukosekana kwa maji kwa siku mbili mfululizo kimesababisha hali ya usafi kuwa
mbaya ukizingatia kwamba nyumba nyingi zinatua vyoo vya ndani.
“Kwa sasa mji wa
Dodoma na maeneo mbalimbali yanakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu hivyo ni
hatari kubwa kukosemaka kwa maji safi,” amesema Mariam.
Mariam alieleza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi kwa wale wenye
watoto wadogo kwani nguo za kuwabadilisha zimekuwa zikichafuka huku hakuna
jinsi yoyote ya kufanya usafi.
Akitoa ufafanuzi
wa jambo hilo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa, Mhandisi Kashilimu Mayunga
amesema tatizo hilo linatokana na kuwepo kwa matatizo ya umeme ambao umekuwa
ukikatwa na Tanesco.
Alisema hali hiyo
katika mji wa Dodoma imesababisha wananchi kukosekana kwa maji na hivyo
kuwashauri wale wenye vifaa kuweka maji ya akib
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment