Zinazobamba

ZITTO KABWE AFUATA NYAYO ZA KINA CHEYO,SHIBUDA NA MLEMA UNDUMI LA KUILI WAKE WAZIDI BAINIKA TENA,SOMA HAPO

 Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto

NA KAROLI VINSENT
NJIA anazopitia Kiongozi mkuu wa Chama ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe katika kukubaliana kila mipango na Chama cha Mapinduzi CCM azipishani  njia walizotumia  wanasiasa walipotea nchini  Agustino Mrema,mzee Memosa Cheyo pamoja na John Shibuda.
    Usaliti wa zitto umebainika leo wakati wa Rais John Magufuli alipokuwa analihutubia Bunge ambapo Wabunge wa vyama vya Upinzani wanaunda UKAWA walipolisusia bunge hilo kwa madai ya kutomtambua Rais aliyemaliza mda wake visiwani Zanzibar Dk Mohamed Shein,
      Ambapo Wabunge wa UKAWA kwa pamoja walishiriki kuimba nyimbo wakisema “Maalim Sef  Maalim Sef” nyimbo hizi ndio zikamfanya Spika wa Bunge Job Ndugai kuamulu wabunge wote watoke nje.
         Wabunge wote wa upinzani wakatoka akabaki peke yake Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma mjini.
     Baada kubaki huko kwa Zitto Kabwe kunazidi ibua utata maana Zitto huyo wiki mbili zilizopita alihitisha mkutano na Wanahabari akilaani kinachotokeza Zanzibar kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo ambayo yalimpa ushindi Mgombea wa Chama cha Wananchi CUF,Maalim Sef
         Zitto katika mkutano huo alisema kitendo cha Dk Shein kuendelea kuongoza Zanzibar ni sawa na uhaini na kutakiwa kushitakiwa kama mhaini,
       Lakini la ajabu Zitto huyo alisema Shein amevunja Katiba ya Zanzibar kuwepo madarakani,lakini leo Bungeni ameungana na hao aliowaita wahaini,
      Akizungumzia hali hiyo,Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Mlimani,Ally Rashid amesema ni wakati watu wakigoma kumtambua zitto kwa sura ya CCM.
“Huyu bwana(Zitto) hana tofauti na kina Mrema,Cheyo,Shibuda maana ni watu ambao wanafanya siasa za kuuma uma tu,maana alimsema Shein ni mhaini sasa leo aliyemuita mhaini leo ameungana nae ndio watu wamjua undimi la kuili wa mwanasiasa huyu”amesema Rashindi

        Zitto Kabwe ambaye kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo alikuwa Kiongozi ndani ya Chadema na alifukuzwa kwenye chama hicho baada ya kubainika alikuwa anapanga mipango ya kukihujuma chama hicho katika harakati zake za ukombozi wa Taifa.








Maoni 3

Unknown alisema ...

Huyo kakomaa kisiasa...walotoka wamesaidika na nn

sipe vic alisema ...

Kumbe wakitoka bungeni ndo ina maana kwmba shein si rais,mkajipange kelele wala fujo si tija,nendeni mkasome somo la majadiliano ya mezani katika kutatua migogoro

Abdallah the Write alisema ...

Karoli Vicent mtu ninayekutambua kama msomi wa taaluma ya habari katika chuo kikuu huria andiko lako la ajabu lisilokidhi taaluma ya habari linazidi kukushusha

Nakuahidi na kukuhakikishia kama utabaki katika uandishi wa aina hii utaendelea kuwa mwandishi wa kuitwa katika makongamano yanayoishia kukupatia elfu 10

Hii ni kutokana na uwezo wako mdogo wa kuchanganua mambo, bahati mbaya hujipi muda wa kufikiri nini unataka kuandika bali unataka uonekane umekuwa wa kwanza kuandika

Mfano wako wa kumuhusisha Zitto kabwe na hao uliowataja haujakidhi vigezo vya Uchan=mbuzi bali ushabiki/mahaba yaliyojengwa katika kutaka sifa usizostahili

Ninakuhurumia mdogo wangu mwanzo ulipofukuzwa Tanzania Daima nilijua wamekuonea kumbe walikuwa sahihi kukufukuza kwa kuwa huzingatii miiko ya uandishi bali ujuaji uliopitiliza
Fikra zako umezielekeza kutaka kila kinachofanywa na unaowashabikia basi kila mmoja akifuate hii si akili ya kawaida ya mwanaadam mwenye kufikiri ninashukuru Mungu rafiki zako kina Exaud wameona upungufu wako huu na sasa hawakupi blog zao uzipostie ujinga wa aina hii