ZITTO KABWE AFUATA NYAYO ZA KINA CHEYO,SHIBUDA NA MLEMA UNDUMI LA KUILI WAKE WAZIDI BAINIKA TENA,SOMA HAPO
NA KAROLI
VINSENT
NJIA anazopitia Kiongozi mkuu wa Chama
ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe katika kukubaliana kila mipango na Chama cha Mapinduzi
CCM azipishani njia walizotumia wanasiasa walipotea nchini Agustino Mrema,mzee Memosa Cheyo pamoja na John
Shibuda.
Usaliti wa
zitto umebainika leo wakati wa Rais John Magufuli alipokuwa analihutubia Bunge
ambapo Wabunge wa vyama vya Upinzani wanaunda UKAWA walipolisusia bunge hilo kwa
madai ya kutomtambua Rais aliyemaliza mda wake visiwani Zanzibar Dk Mohamed
Shein,
Ambapo
Wabunge wa UKAWA kwa pamoja walishiriki kuimba nyimbo wakisema “Maalim Sef Maalim Sef” nyimbo hizi ndio zikamfanya Spika
wa Bunge Job Ndugai kuamulu wabunge wote watoke nje.
Wabunge
wote wa upinzani wakatoka akabaki peke yake Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa
Kigoma mjini.
Baada
kubaki huko kwa Zitto Kabwe kunazidi ibua utata maana Zitto huyo wiki mbili
zilizopita alihitisha mkutano na Wanahabari akilaani kinachotokeza Zanzibar kwa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo ambayo yalimpa ushindi Mgombea wa
Chama cha Wananchi CUF,Maalim Sef
Zitto
katika mkutano huo alisema kitendo cha Dk Shein kuendelea kuongoza Zanzibar ni
sawa na uhaini na kutakiwa kushitakiwa kama mhaini,
Lakini
la ajabu Zitto huyo alisema Shein amevunja Katiba ya Zanzibar kuwepo
madarakani,lakini leo Bungeni ameungana na hao aliowaita wahaini,
Akizungumzia
hali hiyo,Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Mlimani,Ally
Rashid amesema ni wakati watu wakigoma kumtambua zitto kwa sura ya CCM.
“Huyu bwana(Zitto) hana tofauti na kina Mrema,Cheyo,Shibuda
maana ni watu ambao wanafanya siasa za kuuma uma tu,maana alimsema Shein ni
mhaini sasa leo aliyemuita mhaini leo ameungana nae ndio watu wamjua undimi la
kuili wa mwanasiasa huyu”amesema Rashindi
Zitto
Kabwe ambaye kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo alikuwa Kiongozi ndani ya Chadema na
alifukuzwa kwenye chama hicho baada ya kubainika alikuwa anapanga mipango ya
kukihujuma chama hicho katika harakati zake za ukombozi wa Taifa.
Maoni 3
Huyo kakomaa kisiasa...walotoka wamesaidika na nn
Kumbe wakitoka bungeni ndo ina maana kwmba shein si rais,mkajipange kelele wala fujo si tija,nendeni mkasome somo la majadiliano ya mezani katika kutatua migogoro
Karoli Vicent mtu ninayekutambua kama msomi wa taaluma ya habari katika chuo kikuu huria andiko lako la ajabu lisilokidhi taaluma ya habari linazidi kukushusha
Nakuahidi na kukuhakikishia kama utabaki katika uandishi wa aina hii utaendelea kuwa mwandishi wa kuitwa katika makongamano yanayoishia kukupatia elfu 10
Hii ni kutokana na uwezo wako mdogo wa kuchanganua mambo, bahati mbaya hujipi muda wa kufikiri nini unataka kuandika bali unataka uonekane umekuwa wa kwanza kuandika
Mfano wako wa kumuhusisha Zitto kabwe na hao uliowataja haujakidhi vigezo vya Uchan=mbuzi bali ushabiki/mahaba yaliyojengwa katika kutaka sifa usizostahili
Ninakuhurumia mdogo wangu mwanzo ulipofukuzwa Tanzania Daima nilijua wamekuonea kumbe walikuwa sahihi kukufukuza kwa kuwa huzingatii miiko ya uandishi bali ujuaji uliopitiliza
Fikra zako umezielekeza kutaka kila kinachofanywa na unaowashabikia basi kila mmoja akifuate hii si akili ya kawaida ya mwanaadam mwenye kufikiri ninashukuru Mungu rafiki zako kina Exaud wameona upungufu wako huu na sasa hawakupi blog zao uzipostie ujinga wa aina hii
Chapisha Maoni