WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KUKUTANA NA WADAU WA VIWANDA NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Uledi Mussa akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kuhusu siku ya maonesho ya kimataifa ya Kaizen |
KATIKA kuhakikisha sekta ya viwanda
inakuwa na kuleta tija kwa taifa katika uchumi Tanzania inatarajia kukutana na
wadau mbalimbali katika kuadhimisha siku ya Kaizen Inayotarajiawa kuadhishwa 30
Novembar mwaka huu .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Katika maadhimisho hayo yasiku kaizen
yanalenga juu yautekelezaji wa dhana mbalimbali zilizojengwa na wanafalsafa
huyo wakutoka nchini Japan ambapo watalamu mbalimbali wasekta hiyo ya viwanda
katika kujenga uchumi kutokana na sekta ya viwanda .
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na
biashara Uledi Mussa amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha
wataalamu wa sekta hiyo katika kukuza ubora wa bidhaa na kuongeza tija .
‘’Dhana ya kaizen tunatarajia kuitekeleza ambapo asili ya dhana hii
nikutoka nchini Japan ,nchi hii imeweza kukua katika viwanda kwakutekeleza
dhana hii nasisi Tanzania tutashirikiana na nchi ya Japan katika kutekeleza
dhana hii ‘’Amesema Katibu Mkuu Uledi Mussa.
Wanahabari wakiwa kazini wakimsikiliza Katibu mkuu, |
Mussa amesema kuwa dhana hiyo ya KAIZEN inatarajiwa kutekelezwa katika
mikoa mitatu ambayo ni Dar es salaam ,Morogoro ,pamoja na DODOMA .
Ameongeza kuwa katika utekelezaji wadhana hiyo ya KAIZEN
inalenga kukuza sekta binafsi za viwanda ambapo viwanda vyandani ya nchi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni