MPANGO WA MAGUFULI KUPAMBANA NA VIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA,MAASKOFU NA MASHEHE WAIBUKA NAO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Rais wa Tanzania,John Pombe Magufuli |
RAIS mpya wa
Tanzania, Dk. John Magufuli ameambiwa kama ni kweli amenuia kukomesha biashara
ya madawa ya kulevya nchini, basi awashughulikie wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza
bidhaa hiyo. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).
Anaweza kuanza kwa kuifanyia kazi orodha ya
wafanyabiashara 104 magwiji wa madawa hayo, orodha ambayo alipewa mtangulizi
wake, rais mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia madarakani Desemba 2005.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa
jamii ya madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga amesema orodha
hiyo iliguswaguswa tu na uongozi uliopita.
“Sisi viongozi maaskofu na masheikh 120 tuliokutana kwa siku
tatu mjini Arusha kwa lengo la kutathmini athari za tatizo la matumizi ya
mihadarati kwenye Nchi za Maziwa Makuu, tunampongeza Rais John Magufuli
kwa kuweka wazi ajenda ya kupambana na janga hili nchini. Tunamhimiza
aishughulikie ile orodha tuliyomkabidhi mtangulizi wake,” amesema Askofu
Mwamalanga.
Hayo yamo katika tamko la kongamano lililoshirikisha viongozi wa
dini wa nchi za kanda ya Maziwa Makuu kwa ushirikiano wa mashirika ya kidini ya
Ujerumani, Marekani na Afrika yanayopambana na biashara ya usafirishaji, usambazaji,
utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana katika nchi za Ulaya na
kanda hii ya Kusini mwa Afrika.
“Tunaungana naye katika kusimamia ajenda aliyoitangaza katika
hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 11; tunadhani wakati umefika awezeshwe
kutungwa sheria ya adhabu ya kifo ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa wa
‘unga’ kama ilivyo nchini China. Atakuwa ametoa mchango muhimu katika kupunguza
uharibifu unaofanywa dhidi ya maelfu kwa maelfu ya vijana wa Afrika, wakiwemo
Watanzania.
Askofu Mwamalanga wa Kanisa la Kiinjili la
Kipentekoste ameonya Tanzania ni muathirika mkubwa wa tatizo hilo kwa
miaka mingi sasa kama ilivyo kwa janga la rushwa na ufisadi, na kusisitiza
panahitajika sheria hiyo ishikiliwe kwa uimara.
Amesema hotuba za maneno matupu haziwezi kutokomeza rushwa na
biashara ya mihadarati kwani wamiliki wakubwa ni watu wenye utajiri mkubwa
kwa hivyo moyo alioonesha rais mpya utakuwa ukombozi.
Mwanzoni mwa mwaka 2006, Kamati ya Maadili, Amani na Haki za
Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini ilikutana na Kikwete
na kumkabidhi orodha ya magwiji 104 wa mihadarati “kiukweli hapajawa
na mafanikio kwani leo miji yote Tanzania vijana wanafanyabiashara hiyo
kama njugu.”
Askofu Stave Marks na Profesa George Furhaman kutoka Ujerumani
wametambua mchango wa Kamati ya Askofu Mwamalanga wa kukabidhi orodha ya
magwiji wa mihadarati kwani Tanzania haipaswi kutumiwa kama uchochoro wa
kupitisha bidhaa hiyo kwa asilimia 11 kwenda nchi za Kusini mwa Afrika na
Ulaya.
Orodha hiyo inajumuisha majina ya watu waliokuwa wakitumia
mgongo wa vyeo na nafasi zao serikalini na pia ukaribu wao na viongozi wakuu na
marais wa mataifa mbalimbali ya Afrika Tanzania wakiwemo
maaskofu, wachungaji, manabii na masheikh wa uongo.
Mbele ya kongamano hilo, Padre kutoka Zambia alikiri kuwahi kuwa
kinara wa mtandao mahsusi wa kusafirisha madawa ya kulevya kupitia Dar es
Salaam, Tunduma, Lusaka na kuingia Afrika Kusini kati ya mwaka 2005 na 2007.
Alidai kuiacha kazi hiyo baada ya kubaini kuwa jina lake
lilikuwemo kwenye orodha aliyokabidhiwa Kikwete mwaka 2006 na amesema walioamua
kuacha kama yeye ni “mashujaa kwani wengi wao wameishia kunyongwa
nchini China.”
Masheikh Abdallah Zuberi wa Mombasa na Kassimu Mohmed wa
kisiwani Pemba ameitaja Zanzibar kama kitovu kikubwa cha mihadarati kwenye ukanda
huu kutokana na usimamizi dhaifu wa sheria.
Sheikh Mohamed amesema kama jitihada za kudhibiti viongozi
wakubwa wanaoendeleza biashara hiyo zitaachwa kwenye ahadi za wanasiasa walioko
madarakani, ipo hatari kwa nchi nyingi za Afrika kuongozwa na magwiji wa
‘unga’ hasa kwa kuwa safari hii wapo baadhi yao wameshinda uchaguzi mkuu na
kuingia bungeni.
Amewataja watu wanane alioita mapapa wa biashara hiyo wanaoishi
Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar, aliosema wamewatia mfukoni viongozi wakubwa
waliochaguliwa ndipo serikali ikabaki kuhimiza tu katika danganya toto huku
ikiichezea orodha
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni