MPAMBE WA LOWASSA APATA PIGO CHUO KIKUU CHA UDOM,AONDOLEWA,SOMA HAPO KUJUA
Balozi Juma Mwapachu |
BALOZI Dk.
Agustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) kutokana na aliyekuwa ameshika nafasi hiyo Balozi Juma Mwapachu
kumaliza muda wake. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alitoa kauli hiyo leo alipozungumza na
wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mahafari ya chuo hicho
yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 na 27 mwaka huu.
Amesema kuwa Balozi
Mwapachu amemaliza muda wake tangu Oktoba 30 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa Balozi Mahiga ni mzoefu katika utumishi na
amefanya kazi nzuri nje na ndani ya nchi huku akiwa na matumaini makubwa kwamba
ataliongoza baraza hilo bila hofu yeyote.
Hata hivyo amesema
Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amemuongezea
muda wa miezi sita, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala,
Profesa Shaban Mlacha ambaye alipaswa amalize muda wake Desemba 30, mwaka huu.
Amesema, uamuzi wa
kumuongezea muda Profesa Mlacha, umetokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi
ambayo ilianza chini ya uongozi wake ukiwemo mradi wa umeme jua ambayo ameona
abaki ili angalau aifikishe mahali pazuri.
“Profesa Mlacha na
Naibu Makamu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Ludovick Kinabo waliongezewa
muda walioongezewa unaisha Desemba 30 mwaka huu, lakini Mlacha ataendelea
kuwepo kwani ameongezewa miezi sita mingine ili asogeze miradi aliyoianzisha,”
amesema Profesa Kikula.
Kuhusu mahafali
amesema, jumla ya wahitimu 4,136 wa kada na ngazi mbalimbali watatunukiwa vyeti
idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na
wahitimu 3,949.
Amesema, tangu
kuanzishwa kwa chuo, idadi ya wahitimu kuanzia mahafali ya kwanza mwaka 2010 ni
26,663 huku akisema idadi hiyo ni kubwa hali inayohitaji ubunifu ili vijana
wanaosoma katika chuo hicho waweze kuajiriwa na kujiajiri.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni