BANDARI YA DAR ES SALAAM KINARA WA UINGIZAJI WA KEMIKALI,MKEMIA MKUU WA SERIKALI AFUNGUKA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkemia mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele |
BANDARI ya Dar es Salaam imetajwa kuwa ni kinara wa
uingizaji wa kemikali nchini kuriko mahari pengine.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo,
Hayo
yemesemwa leo Jijini Dar Es Salaam na Mkemia mkuu wa Serikali na msajili wa
Kemikali za majumbani pamoja na Viwandani,Profesa Samwel Manyele wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema katika kipindi cha tangu January hadi octoba
mwaka 2015 zimeingizwa kemikali zenye uzito wa tani 472,389,
“Tani hizo zote zinapita kwa wingi kupitia
bandari ya Dar es Salaam ambapo kwa sasa bandari hiyo imeingiza kiasi cha tani 281,468 sawa na asilimia 44”amesema Profesa Manyele.
Sanjari na Bandari ya Dar es Salaam Profesa
manyele ameyataja maeneo mengine yanayoingiza Kemikali ni Mipaka ya Tunduma,Kasumulu,Kasanga,Mtambaswala,Hororo
pamoja na Bandari ya Mtwala,
Amesema katika kupambana na kemili hizo
ambazo baadhi yake zinakuwa na madahara
kwa binadamu,Idara yake imeajili watumishi mbali mbali ambao wamekwenda kwenye
Bandari pamoja na mipaka yote kuhakikisha wanaziangalia na kuzipima kemikali
zote ambazo zitakuwa zinafaa ua zisizo faa kabla hazijafika kwa wananchi,
Pamoja na hayo ofisi hiyo ya Mkemia mkuu
wa serikali imeandaa warsha ambayo inatarajiwa
kuanza kesho kwa wadau mbali mbali wa amasuala ya afya kutoka ndani nchi pamoja
na nje nchi yenye lengo kutoa utafiti mbali mbali.
“ Dhumuni la Warsha hiyo ni Kuwasilisha na
kusambaza matokeo ya utafiti wa kuhamasisha matumizi salama ya kemikali katika
ukanda wa Africa kwa kutumia shughuli za utafiti zilizofanyika katika Bandari
ya Mombasa, Kenya na Tema Ghana”
“Kufundisha nchi za ukanda wa Africa
Mashariki juu ya namna ya kushughulikia na kusimamia kemikali hatari na zenye
madhara, namna ya kujiandaa au kukabiliana matukio ya kemikali pamoja na
kubadilisha uzoefu wa ushughulikiaji salama wa kemikali hizo kati ya nchi na
nchi” amesema Profesa Manyele,
Warsha hiyo ya siku mbili itakayoanza
kesho tarehe 26 na kumalizika siku ya tarehe 27 itafanyika katika hoteli ya
Protea jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni