VITA YA USPIKA YAZIDI KALEA SASA,UKAWA NAO KUTOA SPIKA BORA,SOMA HAPO KUJUA

MBUNGE mteule wa
jimbo la Hai na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
Freeman Mbowe (Chadema) amesema mchakato wa kumpata spika wa Bunge unaendelea
ndani ya umoja huo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Mbali na hilo amesema siyo dhambi kumpata
spika ambaye hatokani na wabunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza waandishi wa
habari juu ya mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la kumi na Moja.
Mbowe alisema mchakato wa uspika ndani ya umoja wao unaendelea
na watakapo maliza wataweka adharani majina ya watu waliochomoza.
Akizungumzia hoja ya Spika kuwa mbunge au la alisema inafaa
zaidi Spika kutokuwa mbunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Amesema kuwa mbunge siyo sifa ya kuwa unakubalika kwani kuna
watu ambao wamekuja bungeni lakini hawakuchaguliwa na wananchi.
“Ninyi waandishi mnajua kuwa uchaguzi ulivyokuwa wapo watu ambao
wamekuja bunge bila kushinda na wengine wametangazwa bila hata kupigiwa kura”.
Alisema
“Inafaa zaidi kama angepatikana spika ambaye hatokani na chama
chochote cha siasa ili kuweza kuondokana na ushabiki wa kulinda maslahi ya
chama fulani.
“Wapo watu wengi ambao siyo wabunge lakini wanaweza kuendesha
vyema bunge jambo ambalo akipatikana spika toka nje ya bunge anaweza kuendesha
bunge vizuri” alisema Mbowe.
Kauli ya Mbowe imetokana na Mbunge mteule wa jimbo la Mtera
Livingston Lusinde (CCM) aliyenukuliwa akisema spika lazima awe mbunge.
Lusinde akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mtu
yoyote ambaye anatoka nje ya hataweza kumpigia kura.
Kwa upande wake Mbunge mteule wa jimbo la Kisarawe Sulemani Jafo
(CCM) alisema spika ambaye atapatikana ni lazima alisimamie vizuri Bunge.
Amesema wananchi wengi wana matarajio makubwa na bunge kwa maana
ya dhana ya mabadiliko.
Mbali na hilo alisema wabunge wanatakiwa kulitumia Bunge kwa
lengo la kuisimamia selikari kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya watanzania
wote bila kujali itikadi za vyama.
“Nataka kuwaambia wabunge wenzangu hususani vijana wahakikishe
wanafanya kazi ya kuisimamia serikali bila kujali itikadi za vyama vyao na wala
kupingana kama vile wanakomoana.
“Pale penye ukweli ni vyema wabunge wote tukakubaliana kwa nia
moja kwa lengo la maslahi mapana ya watanzania wote,” amesema Jafo.
Habari hii kwahisani ya mwanahalis oline
No comments
Post a Comment